Putin: Mazungumzo ya Marais wanaodhamini mchakato wa Astana yalikuwa ya manufaa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i86092-putin_mazungumzo_ya_marais_wanaodhamini_mchakato_wa_astana_yalikuwa_ya_manufaa
Rais Vladmir Putin wa Russia amekitaja kikao cha viongozi wa nchi zinazodhamini mchakato wa Astana kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria kuwa muhimu sasna na kueleza kuwa kikao hicho kilikuwa na maudhui zenye manufaa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 20, 2022 07:26 UTC
  • Putin: Mazungumzo ya Marais wanaodhamini mchakato wa Astana yalikuwa ya manufaa

Rais Vladmir Putin wa Russia amekitaja kikao cha viongozi wa nchi zinazodhamini mchakato wa Astana kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria kuwa muhimu sasna na kueleza kuwa kikao hicho kilikuwa na maudhui zenye manufaa.

Mkutano wa Saba wa wakuu wa nchi zinazodhamini mchakato wa mazungumzo ya Astana ulifunguliwa jana usiku katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa hapa Tehran kwa kuhudhuriwa pia na Ayatullah Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Vladmir Putin wa Russia na Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki.  

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Vladmir Putin jana usiku baada ya kumalizika Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Nchi Zinazodhamini Mchakato wa Astana, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba: taarifa ya mwisho ya mkutano huo kumetiliwa mkazo suala la kuimarisha ushirikiano wa pande tatu kwa ajili ya ukarabati endelevu huko Syria. Aliongeza kuwa, nchi tatu yaani Iran, Russia na Uturuki zimekubaliana kuwa mgogoro wa Syria unaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia tu za kisiasa. 

Marais Rais, Putin na Erdogan katika Mkutano wa mchakato wa Astana mjini Tehran 

Rais wa Russia aidha ameashiria azimio nambari 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na udharura wa kulindwa kikamilifu misingi mikuu ya kuheshimu mamlaka ya kujitawala, umoja wa ardhi nzima na umoja wa taifa la Syria na kueleza kuwa: mustakbali wa Syria unapasa kuainishwa na Wasyria wenyewe bila ya uingiliaji wa nchi ajinabi.  

Rais Putin amedokeza pia kuhusu masuala mengine waliyokubaliana katika mkutano wa Tehran na kueleza kuwa:tumekubaliana kwamba kikao cha 12 cha wataalamu kifanyike mwishoni mwa mwaka huu.