Amir Abdullahian: Maadui wangali wanaendeleza njama mbovu ya kuibua migawanyiko na mifarakano
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe katika Mkutano wa Kwanza wa Kikanda wa Umoja wa Kiislamu na kusema: maadui wangali wanaendeleza njama mbovu ya kuibua migawanyiko na mifarakano.
Mkutano wa Kwanza wa Kikanda wa Umoja wa Kiislamu chini ya anwani "Kurdistan ni nembo ya kutambuliwa umoja wa Umma wa Kiislamu na kuishi pamoja makabila na dini mbalimbali" umeanza leo Jumatano katika mji wa Sanandaj magharibi mwa Iran.
Kati ya Wageni waalikwa 400, 80 miongoni mwao ni raia wa nchi za nje ambao pia wanashiriki katika mkutano huo.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Hossein Amir- Abdullahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe kwa njia ya video katika mkutano huo akieleza kuwa: maadui wangali wanafuatilia kutekeleza njama zao mbovu za kuibua migawanyiko na mifarakano; na mara hii maadui wamedhihirisha hilo katika kalibu ya vyombo vya habari ili kuibua shaka na shubha miongoni mwa vijana wa Ulimwengu wa Kiislamu; na kati ya vitisho vinavyoukabili Umma wa Kiislamu.
Amir Abdullahian ameongeza kuwa japokuwa Wasuni na Washia siku zote wamekuwa wakitilia maanani pakubwa vitisho na hatari hizo, lakini adui angali anataka kustafidi na ugaidi na kueneza ugaidi wa kitakfiri katika eneo ili kudhihirisha taswira mbovu na potofu kuhusu Uislamu safi wa Nabii Muhammad (s.a.w) na taswira isiyo sahihi kuhusu uadilifu wa kinabii kwa uchupaji mipaka unaokinzana na Uislamu kwa jina la Daesh na ugaidi wa kitakfiri unaosababisha hasara na maafa makubwa kwa miundomsingi ya nchi za Kiislamu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran vile vile ametaja njama nyingine ya maadui kuwa ni kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala bandia wa Kizayuni kwa kustafidi na nchi chahce za Ulimwengu wa Kiarabu, na kueleza kuwa: hatua yoyote inayochukuliwa katika uwanja huo ni sawa kusaliti wazi malengo makuu ya wananchi wa Palestina na kukombolewa Quds Tukufu kutoka katika makucha ya Wazayuni.