-
Raisi: Iran na Turkmenistan zina uhusiano uliokita mizizi
Jun 15, 2022 07:55Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uhusiano wa pande mbili wa nchi hii na Turkmenistan ni wa kidugu na uliokita mizizi.
-
Kwa mara nyingine, Iran yalaani jaribio la UK la kuwahamishia wakimbizi nchini Rwanda
Jun 15, 2022 03:01Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mara nyingine tena amelaani jaribio la Uingereza la kuwahamishia kwa lazima wakimbizi wa nchi hiyo huko Rwanda na kusema kuwa hiyo ni aibu ya kihistoria.
-
Rais Raisi atilia mkazo wajibu wa kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan
Jun 15, 2022 03:01Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, nchi yake haina mipaka katika kustawisha uhusiano wake na Pakistan na kusisitiza kuwa, Iran ina uwezo wa kutosha wa kudhamini mahitaji muhimu ya Pakistan katika nyuga tofauti zikiwemo za mafuta, gesi na umeme.
-
Iran yataka UN ichunguze kukiukwa haki za Mwanadiplomasia Muirani aliyefungwa Ubelgiji
Jun 14, 2022 06:43Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezikosoa Ujerumani na Ubelgiji kutokana na kuendelea kushikiliwa kinyume cha sheria na kufikishwa kizimbani mwanadipolomasia Muirani Assadollah Assadi huku ikitaka Umoja wa Mataifa uchunguze namna haki zake zilivyokandamizwa.
-
Kusimama kidete Iran mkabala wa ubabe na upendaji makuu wa Marekani
Jun 14, 2022 06:01Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusiana na mazungumzo ya nyuklia kwamba: Kila mara upande wa pili wa mazungumzo hayo ulipochukua mkondo wa ubabe na kutaka makuu sisi tulitumia nyenzo, nguvu na uwezo wa taifa ili wahusika watambue kwamba, maslahi na utulivu wa taifa la Iran ni jambo lenye umuhimu kwetu.
-
Shirika la Nishati ya Atomiki Iran: Hakuna mada yoyote ya nyuklia nchini ambayo haijatolewa maelezo
Jun 14, 2022 03:40Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran AEOI limetangaza kuwa hakuna mada yoyote ya nyuklia nchini ambayo haijatolewa maelezo; na madai ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA yametokana na taarifa zisizo sahihi na za kubuni ulizopewa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambao wenyewe unamiliki silaha za nyuklia.
-
Rais wa Venezuela atembelea Bustani ya Teknolojia ya Pardis nchini Iran
Jun 13, 2022 22:06Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ametembelea Bustani ya Teknolojia ya Pardis iliyoko katika mji mkuu wa Iran, Tehran na kujionea ustawi mkubwa wa Iran katika sekta ya sayansi na teknolojia.
-
Wabunge wa Iran: IAEA imepoteza itibari ya kiufundi
Jun 13, 2022 06:28Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imesema hatua ya Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ya kupasisha azimio dhidi ya Iran imeonesha wazi kuwa taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imepoteza itibari yake ya kiufundi.
-
Khatibzadeh: Safari ya Rafael Grossi Israel ni pigo kwa itibari ya wakala wa IAEA
Jun 13, 2022 03:37Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kusikitishwa kwake na safari ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) huko Israel na kueleza kwamba, safari hiyo imetoa pigo baya kwa itibari na hadhi ya wakala huo.
-
Raisi: Mataifa ya wanamapambano yana nguvu kubwa za kusambaratisha vikwazo vya Marekani
Jun 12, 2022 23:08Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya Tehran ya kutengeneza meli kubwa ya mafuta na kuikabidhi kwa Venezuela imethibitisha kivitendo kuwa mataifa ya wanamapambano yana nguvu kubwa za kuweza kusambaratisha vikwazo vya Marekani.