Iran yataka UN ichunguze kukiukwa haki za Mwanadiplomasia Muirani aliyefungwa Ubelgiji
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezikosoa Ujerumani na Ubelgiji kutokana na kuendelea kushikiliwa kinyume cha sheria na kufikishwa kizimbani mwanadipolomasia Muirani Assadollah Assadi huku ikitaka Umoja wa Mataifa uchunguze namna haki zake zilivyokandamizwa.
Katika Barua kwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Kazem Gharibabadi Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran ametoa wito kwa taasisi hiyo ya kimataifa iziwajibishe nchi hizo mbili kutokana na kukiuka haki za binadamu za Assadi.
Pamoja na kuwa mwanadiplomasia huyo wa Iran aliyekuwa na makao yake Vienna Austria ana kinga ya kidiplomasia, lakini alikamatwa akiwa safarini Ujerumani Julai 2018 kwa tuhuma bandia.
Miezi mitatabu baada ya kukamtwa, Assadi alipelekwa Ubelgiji na kufunguliwa mashtaka bandia na sasa anahudumu kifungo cha miaka 20 jela.
Katika barua yake, Gharibabadi ameelaani hatua zilizochukuliwa na Ujerumani na Ubelgiji dhidi ya Assadi na familia yake, na kutaja hatua hizo kuwa ni 'ukiuaji wa wazi' wa majukumu ya kimataifa ya nchi hizo.
Afisa huyo wa ngazi za juu amesema Assadi aliteswa vibaya akiwa kizuizini Ujerumani ambapo aliwekwa kwenye seli zenye baridi kali bila mavazi ya kutosha, alinyimwa chakuka kinachofaa na aliwekwa pamoja na wahalifu hatari mbali na mateso mengine mengi aliyopitia mikononi mwa maafisa wa gereza.

Aidha alinyimwa idhini ya kuonana na familia yake katika siku 53 alizoshikiliwa Ujerumani jambo ambalio ni ukiukaji wa wazi wa haki za kimataifa, za kiraia na kisiasa.
Wataalamu wa kisheria wanasema madai dhidi ya Assadi hayana msingi wowote na ni propaganda za kisiasa dhidi ya Iran. Wakuu wa Ubelgiji wanadai kuwa Assadi alipanga njama ya kushambulia wafuasi wa kundi la kigaidi la MKO linalopinga mfumo wa Kiislamu wa Iran. Hata hivyo wakuu wa Iran wamekanusha tuhuma hizo na kuzitaja kuwa zisizo na msingi.
Kundi la kigaidi la MKO ambalo limepewa hifadhi katika nchi nyingi za Ulaya limetekeleza hujuma za kigaidi ambazo zimepelekea Wairani zaidi ya 12,000 kupoteza maisha tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.