-
Iran: Haki za binadamu ni wenzo wa kisiasa unaotumiwa kwa ajili ya kusukuma mbele malengo ya madola makubwa
May 16, 2022 03:18Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, suala la haki za binadamu limegeuzwa kuwa wenzo wa kisiasa wa madola makubwa kwa ajili ya kusukuma mbele gurudumu la malengo yao.
-
Raisi akutana na ulamaa wa Ahul Sunna Iran, asisitiza umoja wa Shia na Sunni
May 15, 2022 23:12Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na maulamaa na wanazuoni wa Ahul Sunna wal Jamaa nchini Iran na kusisitiza kwamba umoja wa Shia na Sunni ni suala la kimkakati.
-
Bagheri Kani: Siasa za kiistratijia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufelisha vikwazo
May 15, 2022 07:39Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, siasa za kimkakati za Jamhuri ya Kiislamu ni kufelishi vikwazo.
-
Iran yalaani ukiukwaji mpya wa haki za binadamu uliogundulika Marekani
May 15, 2022 06:31Kazem Gharibabadi, Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa taarifa baada ya uchunguzi kubaini vifo vya zaidi ya watoto 500 wa jamii za asili za Marekani katika shule za bweni za kanisa, zilizofadhiliwa na serikali na kusema: "Pamoja na kuwepo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huko Marekani nchi hiyo inajipa jukumu la kuwapa wengine nasaha kuhusu haki za binadamu."
-
Spika: Siku ya Nakba inakumbusha uvamizi, mauaji ya kimbari, ukatili na jinai za Wazayuni
May 15, 2022 03:39Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran, Bunge amesema: Siku ya Nakba inakumbusha uvamizi, mauaji ya kimbari, ukatili na jinai za Wazayuni.
-
Makomandoo wa Iran wazima hujuma ya maharamia Ghuba ya Aden
May 14, 2022 22:04Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuwa makomandoo wa jeshi hilo wamezima hujuma ya maharamia dhidi ya meli ya kibiashara ya Iran katika Ghuba ya Aden.
-
Wasichana wa Afghanistan wakimbilia Iran kupata masomo baada ya Taliban kuwazuia kusoma
May 14, 2022 21:52Idadi kubwa ya familia za Afghanistan zinakimbilia Iran baada ya serikali ya Taliban kukataa kutekeleza ahadi yake ya kuwaruhusu wasichana waendelee na masomo nchini humo.
-
Iran na Russia zaanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia
May 14, 2022 06:42Jamhuri ya Kiislamu ya Ira na Russia zimeanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia kwa ajili ya kuendesha miraji ya pamoja ya ustawi na maendeleo katika uga huo.
-
Shamkhani: Mazungumzo ya Vienna yatafunguka iwapo utatuzi wa kimantiki wa Iran utaheshimiwa
May 14, 2022 03:28Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema mazungumzo ya Vienna yamefika awamu ambayo fundo hilo linaweza kufunguliwa iwapo tu ipande uliokiuka makubaliano ya JCPOA utashehimu njia za ufumbuzi wa kimantiki na kwa mujibu wa kanuni.
-
Iran: Njia pekee ya kupatikana haki za Wapalestina ni serikali na wananchi wa mataifa ya Waislamu kuunga mkono Muqawama
May 14, 2022 00:16Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa kwa mnasaba wa kuwadia kumbukumbu ya Siku ya Nakba na kusisitiza kuwa, wananchi na viongozi wa mataifa ya Waislamu inapasa watambue kuwa njia pekee ya kupatikana haki za watu wa Palestina ni kuwepo umoja na mshikamano wa Kiislamu na uungaji mkono wa serikali na wananchi wa mataifa ya Waislamu pamoja na watetezi wa ukombozi duniani kwa Muqawama wa kukabiliana na maghasibu na watumiaji mabavu.