Iran na Russia zaanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83616-iran_na_russia_zaanzisha_kituo_cha_pamoja_cha_teknolojia
Jamhuri ya Kiislamu ya Ira na Russia zimeanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia kwa ajili ya kuendesha miraji ya pamoja ya ustawi na maendeleo katika uga huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2022 06:42 UTC
  • Iran na Russia zaanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia

Jamhuri ya Kiislamu ya Ira na Russia zimeanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia kwa ajili ya kuendesha miraji ya pamoja ya ustawi na maendeleo katika uga huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, nchi mbili za Iran na Russia zina uwezo mkubwa wa kisayansi na kitekonolojia pamoja na ubunifu wa mambo mbalimbali hivyo mashirika ya teknolojia ya Iran yameamua kushirikiana na mashirika kama hayo ya nchini Russia kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kuuziana teknolojia na pia kusafirisha nje bidhaa na huduma za kiteknolojia ambazo ni uvumbuzi wa mara ya kwanza wa nchi hizo mbili ambao haujafanyika sehemu yoyote duniani. 

Kituo hicho kimefungliwa katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Saint Petersburg huko Russia kwa lengo la kutia kasi maendeleo ya kisayansi na kitekonolojia ya nchi hizo mbili.

Muonekano wa karibu wa Chuo cha Ufundi cha Saint Petersburg nchini Russia

 

Chuo hicho cha Russia ni katika vyuo vikuu vya daraja la kwanza duniani na sasa hivi kinasimamia na kuendesha miradi kadhaa ya kitaifa ya teknolojia ya kisasa.

Kituo hicho cha pamoja cha teknolojia cha Iran na Russia kina uongozi wa kujitegemea na kina kumbi za pamoja kubwa za kuendesha semina na vikao mbalimbali na pia kina nafasi ya kuendesha masomo ya pamoja ya teknolojia. Kimetengewa nafasi pia ya kuimarisha mashirika ya elimu msingi pamoja na masuala ya uvumbuzi na ubunifu katika sekta tofauti zenye manufaa kwa mataifa haya mawili na duniani kwa ujumla.