Shamkhani: Mazungumzo ya Vienna yatafunguka iwapo utatuzi wa kimantiki wa Iran utaheshimiwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83600-shamkhani_mazungumzo_ya_vienna_yatafunguka_iwapo_utatuzi_wa_kimantiki_wa_iran_utaheshimiwa
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema mazungumzo ya Vienna yamefika awamu ambayo fundo hilo linaweza kufunguliwa iwapo tu ipande uliokiuka makubaliano ya JCPOA utashehimu njia za ufumbuzi wa kimantiki na kwa mujibu wa kanuni.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
May 14, 2022 03:28 UTC
  • Ali Shamkhani
    Ali Shamkhani

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema mazungumzo ya Vienna yamefika awamu ambayo fundo hilo linaweza kufunguliwa iwapo tu ipande uliokiuka makubaliano ya JCPOA utashehimu njia za ufumbuzi wa kimantiki na kwa mujibu wa kanuni.

Duru ya nane ya mazungumzo ya kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran ambayo ilianza Disemba 27 mwaka jana, ilisitishwa kwa pendekezo lililotolewa na Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya; ambapo timu za mazungumzo zilirejea katika miji yao mikuu kwa mashauriano zaidi. 

Tokea wakati huo hadi sasa, pande husika katika mazungumzo hayo, yaani kundi la nchi za 4+1 ambazo ni  China, Russia, Uingereza, Ufaransa pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwa upande wa pili zimekuwa zikizungumza kuhusu suala la kupunguza hitilafu. Kilichobakia ni kuwaondoa watu na taasisi katika orodha ya vikwazo; ambapo  Marekani, ikiwa nchi iliyokiuka na kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, haijachukua maamuzi ya kisiasa kuhusu kadhia hii. 

Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran aliandika jana katika ukurasa wake wa Twitter kwamba:  Marekani kwa kutotekeleza majukumu yake, na Ulaya kwa kutowajibika kivitendo, zimevuruga fursa ya kunufaika na nia njema iliyodhihirishwa na Iran; na kama pande hizo zitakuwa na azma ya kweli ya kurejea kwenye JCPOA, basi Iran iko tayari kufikia mapatano. 

Enrique Mora Mratibu wa Mazungumzo ya Vienna Jumatano na juzi Alhamisi alikutana hapa Tehran Ali Bagheri Kani, kiongozi wa ujumbe wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia ambapo pande mbili zilizungumzia suala la kuendeleza mazungumzo ya Vienna. 

Ali Bagheri Kani katika mazungumzo na Enrique Mora 

Jana pia Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya (EU) alisema mazungumzo ya kuindolea Iran vikwazo ilivyowekewa na Marekani yataanza tena siku chache zijaz.; Ameitaja safari ya Enrique Mora mjini Tehran kuwa chanya  na kuongeza kuwa, mazungumzo na Iran yatazamiwa kuanza tena hivi karibuni.