Wasichana wa Afghanistan wakimbilia Iran kupata masomo baada ya Taliban kuwazuia kusoma
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83624-wasichana_wa_afghanistan_wakimbilia_iran_kupata_masomo_baada_ya_taliban_kuwazuia_kusoma
Idadi kubwa ya familia za Afghanistan zinakimbilia Iran baada ya serikali ya Taliban kukataa kutekeleza ahadi yake ya kuwaruhusu wasichana waendelee na masomo nchini humo.
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
May 14, 2022 21:52 UTC
  • Wasichana wa Afghanistan wakimbilia Iran kupata masomo baada ya Taliban kuwazuia kusoma

Idadi kubwa ya familia za Afghanistan zinakimbilia Iran baada ya serikali ya Taliban kukataa kutekeleza ahadi yake ya kuwaruhusu wasichana waendelee na masomo nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Press TV, wasichana wengi wa Afghanistan wamepata hifadhi Iran ili kuendelea na masomo katika mwaka mpya wa masomo ambao umeanza Machi.

Baada ya kuchukua madaraka mwaka jana kufuatia kuondoka kwa madhila Marekani nchini Afghanistan, kundi la Taliban limekuwa likitoa ahadi ya kuwahakikishia wasichana kuwa wataweza kuendelea na masomo shuleni lakini kundi hilo limebatilisha uamuzi huo na sasa maelfu ya wasichana hawawezi kuendelea na masomo nchini humo.

Askari wa Taliban waliwekwa nje ya shule kote Afghanistan na kuwafanya wasichana iwalazimu warejee majumbani.

Kufuatia uamuzi huo wa utawala wa Taliban,  idadi kubwa ya wasichana wa Afghanistan wamekimbilia Iran hasa katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa nchi na sasa wameanza masomo yao.

Mwaka jana Filippo Grandi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) aliipongeza Iran kwa ukarimu wake mkubwa katika kuwapa huduma wakimbizi hasa wale waliodhulumiwa kutoka nchi jirani ya Afghanistan.

Askari wa Taliban akilinda doria

Mwaka 2015, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, alisema hivi kuhusu haki ya kupata elimu watoto wakimbizi kutoka Afghanistan hata wale ambao wako nchini kinyume cha sheria: "Mtoto Muafghani, hata yule ambaye yuko Iran kinyume cha sheria na bila nyaraka zozote, hapaswi kunyimwa fursa ya kujiendeleza kimasomo na wote wanapaswa kusajiliwa katika shule za Iran."

Agizo hilo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu ulazima wa watoto wote Waafghani nchini Iran kupata elimu katika shule za serikali ni kati ya sera bora zaidi za kuwahudumia wakimbizi na sera kama hiyo ni ya aina yake na ya kipekee duniani.