-
Rais wa Iran alaani jinai iliyofanywa na mkufurishaji mmoja dhidi ya Masheikh katika Haram ya Imam Ridha AS
Apr 06, 2022 02:45Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai iliyofanywa na mtu mmoja mkufurishaji katika Haram tukufu ya Imam Ridha AS na kusema kuwa, aliyefanya jinai hiyo ni mtu mpotofu aliyeathiriwa na magenge ya ukufurishaji ya Kimarekani.
-
Iran: Tuko tayari kuisaidia Afghanistan kulima mazao ya chakula badala ya mihadarati
Apr 05, 2022 22:21Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Afghanistan umesema kuwa, Tehran iko tayari kuisaidia Afghanistan kulima mazao ya chakula badala ya mmea wa mpopi unaozalisha mihadarati na madawa haramu ya kulevya.
-
Iran haiwezi kusalimu amri mbele ya kujitakia makuu Marekani
Apr 04, 2022 22:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu katu haiwezi kusalimu amri mkabala wa uchu, tamaa na kujitakia makuu Marekani.
-
Khatibzadeh: Iran inafanya juhudi za kufikisha kwa walimwengu vilio vya watu wa Yemen
Apr 04, 2022 21:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran imepokea vizuri usitishaji vita wa miezi miwili huko Yemen na kwamba Tehran inafanya juhudi za kufikisha kwa walimwengu vilio vya wananchi wa nchi hiyo, kadiri inavyowezekana.
-
Iran iko tayari kuisaidia Qatar kuandaa Kombe la Dunia kwa mafanikio
Apr 04, 2022 07:14Katika mazungumzo ya simu na Amir wa Qatar, Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu Iran amesisitiza utayarifu wa Iran katika kuisaidia nchi hiyo kuandaa kwa mafanikio Kombe la Dunia.
-
Mpira wa mazungumzo ya Vienna kwenye uwanja wa Marekani
Apr 04, 2022 06:31Katika mazungumzo yake ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuondolewa vikwazo huko Vienna, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu imewasilisha mapendekezo yake kwa Marekani kuhusu masuala yaliyosalia kupitia mpatanishi mkuu wa Umoja wa Ulaya."
-
Amir Abdollahian: Marekani inabeba dhima moja kwa moja kutokana na kuchukua muda mrefu mazungumzo ya Vienna
Apr 04, 2022 02:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa hatua ya Marekani ya kuwawekea vikwazo vipvya baadhi ya shakhsiya na mashirika ya Iran na kueleza kuwa Marekani inabeba dhima moja kwa moja kutokana na kuchukua muda mrefu mazungumzo ya Vienna.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Sanaa ya qiraa ya Qur'ani ihudumie dhikri na ulinganiaji wa dini ya Mwenyezi Mungu
Apr 03, 2022 22:07Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Ramadhani ni mwezi wa ugeni na rehema zisizo na kikomo za Mwenyezi Mungu, na kwamba kutakasa nafsi, kuanisika kunakoambata na kutafakari kwa kina na kuelewa vyema Qur'ani ni miongoni mwa mambo muhimu yanayomuwezesha mwanadamu kufaidika na ugeni huo wa Mola Karima.
-
Rais wa Iran azitaka nchi za eneo zisipuuze njama za kibeberu za US-Israel
Apr 03, 2022 22:06Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi yoyote katika eneo la Asia Magharibi itayopuuza njama na malengo ya kibeberu ya Marekani na utawala wa Kizayuni, itakuwa imepuuza maslahi ya taifa lake, na itaandamwa na ghadhabu za mataifa ya Kiislamu.
-
Amir Abdollahian azungumza kwa simu na Guterres: Mapatano yanakaribia katika mazungumzo ya Vienna
Apr 03, 2022 06:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa mapendekezo ya Iran katika mazungumzo ya Vienna yametumwa upande wa Marekani mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo; na sasa mpira upo mbele ya Marekani.