-
Khatibzadeh: Vikwazo vipya dhidi ya raia wa Iran vinadhihirisha nia mbaya ya Washington
Mar 31, 2022 06:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya raia wa Iran ni ishara nyinine ya nia mbaya ya serikali ya Marekani mkabala wa wananchi wa Iran.
-
Mkuu wa IRGC atahadharisha kuhusu shughuli za Israel katika Ghuba ya Uajemi
Mar 31, 2022 03:30Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amezionya baadhi ya nchi za Kiarabu kwamba uwepo wa Israel katika eneo la kistratijia la Ghuba ya Uajemi ni sababu ya ukosefu wa usalama, na amezitaka zisitishe ushirikiano wao na utawala huo ghasibu.
-
Iran: Utawala wa Kizayuni ndio tatizo kuu la Ulimwengu wa Kiislamu
Mar 30, 2022 21:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio tatizo kuu la Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Khatibzadeh: Bara la Afrika lina nafasi maalumu katika siasa za nje za Iran
Mar 30, 2022 07:18Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema kuwa bara la Afrika lina nafasi ya juu kabisa katika siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ershadi: Vikwazo vinatishia haki ya tiba ya wananchi wa Iran
Mar 30, 2022 02:16Balozi na Naibu Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema vikwazo vya upande mmoja vya Marekani ni tishio kubwa kwa haki ya kupata huduma za afya, matibabu na dawa wananchi wa Iran.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran awasili China kushiriki mkutano kuhusu Afghanistan
Mar 29, 2022 22:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewasili nchini China kwa ajili ya kushiriki kwenye kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazopakana na Afghanistan. Mara baada ya kuwasili nchini humo Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye Twitter kuwa, Iran na China zinaunga mkono uhuru, umoja wa kitaifa na haki ya wananchi wa Afghanistan ya kujiamulia wenyewe mambo yao.
-
Iran yakaribisha mpango wa suluhu uliobuniwa na Mkuu wa Baraza Kuu la Yemen
Mar 29, 2022 03:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekaribisha mpango wa suluhu uliopendekezwa na Mkuu wa Baraza Kuu la Yemen wa kutangaza usitishaji vita wa upande mmoja.
-
Khatibzadeh: Kufanyika mkutano wa uovu ni usaliti kwa lengo tukufu la ukombozi wa Palestina
Mar 28, 2022 22:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kufanyika mkutano wa uovu Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuuelezea kuwa ni usaliti kwa lengo tukufu la ukombozi wa Palestina.
-
Mkuu wa IRGC: Maadui wanaogopa jibu zito la Iran
Mar 28, 2022 06:39Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amesema kosa lolote dogo katika kuamiliana na Iran litaibua jibu zito, na kwa msingi huo maadui hawana uthubutu na ujasiri wa kuitunishia misuli Jamhuri ya Kiislamu.
-
Uchu wa Marekani wa kuzidi kuvutia maslahi yake; kizuizi kikuu katika mazungumzo ya Vienna ya uondoaji vikwazo
Mar 28, 2022 05:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, katika hatua za mwisho za mazungumzo ya Vienna ya uondoaji vikwazo, Marekani inaibua mambo kadhaa ya kuvutia zaidi maslahi yake.