-
Ayatullah Khamenei: Mwaka 1401 Shamsia ni mwaka wa uzalishaji unaotegemea elimu na kutengeneza ajira
Mar 21, 2022 00:01Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuanza mwaka 1401 Hijria Shamsia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelipongeza taifa kwa kuwadia sikukuu ya Nowruz na kuutaja mwaka mpya kuwa ni mwaka wa "uzalishaji unaotegemea elimu na kutengeneza ajira."
-
Raisi katika ujumbe wa Nowruz 1401: Karne ya 15 ni karne ya Iran ya Kiislamu
Mar 21, 2022 00:00Katika ujumbe wake wa Nowruz na mwaka mpya wa 1401 Hijria Shamsia, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja karne ya kumi na tano Hijria Shamsia kuwa ni karne ya Iran ya Kiislamu na zama za watu wa Iran kuwa na nafasi na machango muhimu zaidi.
-
Kumbukumbu ya kupasishwa sheria ya kutaifishwa sekta ya mafuta ya Iran
Mar 20, 2022 09:55Tarehe 29 mwezi Esfand mwaka 1329 kwa kalenda ya Iran inaadhimishwa kama siku ya kukumbuka kupasishwa sheria ya kutaifishwa sekta ya mafuta ya Iran .
-
Makubaliano ya Vienna hayataifanya Iran iache kufuatilia faili la mauaji ya Soleimani
Mar 20, 2022 04:13Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Idara ya Mahakama ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haitaacha kuwafuatilia wahusika wa mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kwa sababu ya makubaliano ya mazungumzo ya Vienna.
-
Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Undumakuwili kuhusu haki za binadamu ni mwanzo wa mwisho wa nguvu ya Magharibi
Mar 18, 2022 11:30Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia ukandamizaji wa utawala wa Al-Saud na mauaji ya halaiki ya makumi ya vijana nchini Saudi Arabia na kusema undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu ni mwanzo wa mwisho wa nguvu ya Magharibi na kuporomoka mfumo wa ubeberu.
-
Iran: Muelekeo wa kisiasa na wa upendeleo hausaidii kuboresha haki za binadamu
Mar 18, 2022 04:39Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu ripoti ya ripota maalumu wa hali ya haki za binadamu Iran kwa kusisitiza kuwa, muelekeo wa kisiasa na kiupendeleo juu ya haki za binadamu si tu hausaidii kuboresha, bali unaharibu na kudhoofisha haki za binadamu.
-
Kuuawa Luteni Jenerali Soleimani ni pigo kubwa kwa mapambano dhidi ya ugaidi
Mar 17, 2022 23:57Mwakilishi wa Iran katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la umoja wa Mataifa amesema, kitendo cha serikali ya Marekani cha kumuua shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani kilisababisha pigo kubwa kwa mapambano dhidi ya ugaidi wa eneo.
-
Jahromi: Uingereza imesalimu amri mbele ya nguvu za taifa la Iran
Mar 17, 2022 07:25Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, baada ya kupita miaka 40 ya kutotekeleza ahadi zake, hatimaye Uingereza imesalimu amri mbele ya nguvu za mazungumzo za taifa la Iran.
-
Taasisi tano za kimataifa za kitamaduni na kisheria zalaani mauaji ya makumi ya wafungwa Saudi Arabia
Mar 16, 2022 22:51Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as), Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al Mustafa na Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran zimelaani kitendo cha kunyongwa watu 81 kaktika masaa 24 huko Saudi Arabia.
-
Amir-Abdollahian: Ikiwa Marekani itazingatia uhalisia wa mambo tutafikia mwafaka mzuri
Mar 16, 2022 04:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema "ikiwa Marekani itazingatia uhalisia wa mambo tutaweza kufikia mwafaka mzuri, imara na wa kudumu kwa uungaji mkono wa pande zote katika mazungumzo ya Vienna."