-
Gharibabadi: Nchi 3 za Ulaya zimejiondoa zenyewe kwenye diplomasia na Iran
Nov 16, 2025 07:29Naibu Waziri wa Masuala ya Sheria na Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo amesema wakati akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Fars kwamba, Iran itaendelea kuonesha ushirikiano na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kwa mujibu wa hatua zinazochukuliwa na Bodi ya Magavana ya wakala huo na kamwe haitofumbia macho haki yake ya kiimsingi ya kunufaika na teknolojia ya kisasa ya nyuklia.
-
Kutopendelea IAEA upande wowote; takwa kuu la Iran katika kadhia ya nyuklia
Nov 16, 2025 06:54Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuhusu ripoti ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA: "lazima ripoti kama hizo zibaki daima kuwa za kitaalamu, zinazotokana na ukweli halisi, na zisizoathiriwa na utashi wowote wa kisiasa".
-
Msemaji wa serikali ya Iran: Jibu kali zaidi linasubiri uvamizi wowote utakaokaririwa dhidi ya nchi hii
Nov 15, 2025 23:25Msemaji wa serikali ya Iran ameeleza kuwa Iran itatoa jibu kali zaidi na kwa nguvu kubwa" ikilinganishwa na wakati uliopita ikiwa itakabiliwa na na uchokozi mpya wa nchi ajinabi.
-
Watalii zaidi ya milioni 3 wa kigeni watembelea Iran katika muda wa miezi sita
Nov 15, 2025 22:59Waziri wa Turathi za Utamaduni na Utalii wa Iran ametangaza kuongezeka kwa idadi ya watalii wa kigeni wanaoingia na kutembelea Iran.
-
Kikosi cha Wanamaji cha IRGC chakamata meli ya mafuta kusini mwa Makran kwa kukiuka taratibu
Nov 15, 2025 09:35Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limekamata meli ya mafuta katika pwani ya kusini ya Makran baada ya kupokea amri ya mahakama.
-
Amir Saeed Iravani: Kamwe Iran haitasalimu amri mbele ya vitisho
Nov 15, 2025 08:57Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Tehran kamwe haitasalimu amri mbele ya vitisho vya kijeshi, mashinikizo ya kisiasa, au vikwazo vya kiuchumi.
-
Qalibaf: Israel haijawahi kuonja moto kama wa Vita vya Siku 12
Nov 14, 2025 23:07Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kwamba: Israel ilikumbaa na mashinikizo makubwa ya kukabiliana na mashambulizi ya Iran hususan katika siku za mwisho za Vita vya Siku 12 na haijawahi kupata kipigo kama ilichopata wakati wa vita vya siku 12 ilivyovianzisha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Jenerali Hassanzadeh: Mifumo ya ulinzi wa dunia inagwaya mbele ya makombora ya Iran
Nov 14, 2025 23:07Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) mjini Tehran, amezungumzia nguvu zinazozidi kuongezeka za Jamhuri ya Kiislamu za kupambna na madola ya kibeberu duniani na kusema: "Katika vita vya siku 12, mifumo jumuishi ya ulinzi ya kimataifa iligwaya na kuzipigia magoti nguvu za makombora za Iran na adui alihisi kushindwa vitani katika muda usiozidi saa 24.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa Tehran: Vyombo vya kidiplomasia vimfungulie mashtaka Trump mhalifu katika majukwaa ya kimataifa
Nov 14, 2025 07:44Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema vyombo vya kidiplomasia vinapaswa kumfungulia mashtaka Donald Trump mhalifu katika majukwaa ya kimataifa.
-
Iran na Uturuki zatilia mkazo kupunguzwa mivutano na kurejeshwa amani na uthabiti katika eneo
Nov 14, 2025 04:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyidd Abbas Araqchi, amefanya mazunguzmo kwa njia ya simu na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan, ambapo wawili hao wamejadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya kikanda na kimataifa.