Pezeshkian: Ukoloni hauna nafasi katika dunia; Iran yataka mahusiano ya kuheshimiana
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138254-pezeshkian_ukoloni_hauna_nafasi_katika_dunia_iran_yataka_mahusiano_ya_kuheshimiana
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa ukoloni na unyonyaji havitakuwa na nafasi katika dunia ya kesho, akisisitiza tena dhamira ya Iran ya kuendeleza mahusiano ya kirafiki yanayojengwa juu ya kuheshimiana na maslahi ya pamoja.
(last modified 2026-05-09T10:06:25+00:00 )
May 09, 2026 09:27 UTC
  • Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian
    Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa ukoloni na unyonyaji havitakuwa na nafasi katika dunia ya kesho, akisisitiza tena dhamira ya Iran ya kuendeleza mahusiano ya kirafiki yanayojengwa juu ya kuheshimiana na maslahi ya pamoja.

Katika ujumbe aliouandika kwenye X siku ya Ijumaa, Pezeshkian alisema: “Sera ya kudumu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kupanua uhusiano wa kirafiki kwa kuheshimiana na kwa misingi ya maslahi ya pamoja. Sera ya ukoloni na unyonyaji haina nafasi katika dunia ya baadaye.”

Rais Pezeshkian amesisitiza kuwa utambulisho wa Iran umetokana na uvumilivu pamoja na kusimama kidete dhidi ya dhulma.

Ameongeza kuwa: “Kama ambavyo uvumilivu umejikita katika tamaduni za watu wetu, mapambano dhidi ya dhulma yamekuwa yakimulika katika historia ya ardhi hii,” huku akisisitiza kuwa, “Utambulisho huu utaendelea kuinua juu jina la Iran.”

Ujumbe huo unakuja wakati Iran imeweza kustahimili vita viwili vya kichokozi vya Marekani na utawala wa Israel katika kipindi cha mwaka uliopita. Mashambulio ya karibuni—yaliloanzishwa tarehe 28 Februari kupitia mauaji ya maafisa wa ngazi za juu na makamanda wa kijeshi wa Iran, yameua zaidi ya Wairani 3,000 na kuharibu miundombinu ya kiraia katika maeneo mbalimbali nchini.

Jeshi la Iran lilijibu kwa mashambulizi makali dhidi ya kambi na mali za kijeshi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi pamoja na kambi za kijeshi za Israel zilizoko katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Tangu tarehe 28 Februari, Tehran imeweka udhibiti mkali katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, ikizuia meli zinazomilikiwa na wahusika wa uvamizi huo au wale waliounga mkono vita hivyo.

Wakati huohuo, Marekani imeweka mzingiro wa baharini usio halali dhidi ya bandari na meli za Iran tangu Aprili 13, hatua inayokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofanikishwa na Pakistan kati ya Tehran na Washington.

Iran imesisitiza kwamba haitaufungua tena njia hiyo muhimu ya kimkakati iwapo mzingiro wa Marekani unaendelea.