-
Raeisi: Tunataka kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote jirani, haswa Saudi Arabia
Jun 21, 2021 08:13Rais mteule wa Iran amesema kuwa mahudhuria makubwa ya taifa la Iran katika uchaguzi wa rais uliofanyika siku chache zilizopita hapa nchini ni dhihirisho la azma ya wananchi na ujumbe muhimu kwa walimwengu.
-
Rais Rouhani: Magaidi wa Marekani wamekiri kwamba wamefunga shughuli za kibenki za Iran
Jun 21, 2021 05:57Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, magaidi wa Kimarekani wamekiri kikamilifu kwamba wamewafungia Wairani kila kitu zikiwemo shughuli zinazohusiana na masuala ya benki.
-
Iran: Kinachosubiriwa kuhusu mapatano ya JCPOA ni maamuzi ya kisiasa tu
Jun 21, 2021 02:58Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kilichobakia kuhusu mazungumzo ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni maamuzi ya kisiasa tu, na kama wanasiasa watachukua maamuzi sahihi, basi mazungumzo hayo yatakamilika.
-
Vipaumbele vya siasa za serikali ijayo ya Iran kuhusu eneo la Mashariki ya Kati
Jun 21, 2021 00:39Baada ya uchaguzi wa rais wa Ijumaa iliyopita ambao matokeo yake yamempa ushindi Sayyid Ebrahim Raisi, kunajitokeza swali kwamba, siasa za nje za Iran kuhusiana na eneo la Magharibi mwa Asia zitakuwa vipi katika serikali ijayo ya Tehran?
-
Araqchi: Inachotaka Iran ni kuondolewa vikwazo vyote vya Marekani
Jun 20, 2021 22:38Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kwa kusisitiza kwamba inachotaka Tehran ni kufutwa vikwazo vyote vya Marekani na msimamo huo kamwe hautobadilika.
-
Ujumbe wa Uchaguzi wa Iran katika eneo la Asia Magharibi
Jun 20, 2021 22:19Kujitokeza mamilioni ya wananchi wa Iran katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, siku ya Ijumaa ya tarehe 18 Juni 2021 kumetoa ujumbe wa kila namna katika eneo la Asia Magharibi.
-
Rais Rouhani asema rais mteule Raeisi atakabidhiwa ripoti za hali ya uchumi nchini
Jun 20, 2021 08:26Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaamuru wanachama wa Idara ya Kiuchumi wa Serikali kumkabidhi rais mteule Sayyid Ebrahim Raeisi taarifa zote za hali ya kiuchumi ya nchi.
-
Viongozi wa dunia wampongeza Raeisi kwa ushindi katika uchaguzi rais Iran
Jun 20, 2021 07:19Viongozi mbali mbali duniani wanaendelea kumtumia salamu za pongezi Sayyid Ebrahim Raeisi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika Ijumaa.
-
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa kuwashukuru wananchi wa Iran kwa hamasa kubwa waliyoonesha
Jun 20, 2021 04:06Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumamosi, tarehe 19 Juni, 2021 alituma ujumbe muhimu kwa mnasaba wa hamasa kubwa iliyooneshwa na wananchi wa Iran walioshiriki kwa mamilioni katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na amelishukuru taifa la Iran kwa kujenga hamasa hiyo adhimu.
-
Rais Nicolas Maduro apongeza ushindi wa Ayatullah Raisi katika uchaguzi wa Rais
Jun 20, 2021 03:44Rais wa Venezuela ametuma ujumbe akimpongeza Sayyid Ibrahim Raisi kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa rais hapa nchini na ametoa wito wa kuboreshwa zaidi uhusiano kati ya nchi mbili.