Jun 20, 2021 12:56 UTC
  • Rais Hassan Rouhani
    Rais Hassan Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaamuru wanachama wa Idara ya Kiuchumi wa Serikali kumkabidhi rais mteule Sayyid Ebrahim Raeisi taarifa zote za hali ya kiuchumi ya nchi.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo alipokutana na wanachama wa Idara ya Kiuchumi ya Serikali na kusisitiza ulazima wa ripoti hizo kukabidhiwa kwa rais mteule Raeisi.

Aidha amesema sekta zote serikalini zimekuwa zikijitahidi kukabiliana na vikwazo vya maadui wa Iran na kuongeza kuwa, kunafanyika jitihada za kuhakikisha kuwa fedha za kigeni zinatengwa kwa ajili ya kuagiza kutoka nje ya nchi bidhaa zinazohitajika. 

Baada ya uchaguzi wa13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu uliofanyika Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran jana imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo ulioshirikisha mamilioni ya wapiga kura.

Wananchi wakisherehekea ushindi wa Rais Raeisi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abdolreza Rahmani Fazli alitangaza matokeo hayo Jumamosi mbele ya waandishi wa habari hapa jijini Tehran na kusema kuwa, wapiga kura milioni 28 na laki tisa na 36 elfu na nne wameshiriki katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesema, asilimia 48.8  ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura wameshiriki kwenye uchaguzi huo. Ameongeza kuwa, Sayyid Ebrahem Raeisi ndiye aliyechaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kura milioni 17 na laki 9 na 25,345 za wananchi.

Rais Rouhani ambaye amemaliza muhula wake wa pili ataendelea kushikilia nafasi ya urais kwa muda wa takribani siku 45 kabla ya Raeisi kuapishwa kuchukua rasmi hatamu za uongozi. Katika kipindi hicho cha mpito serikali iliyoko madarakani hukabidhi taarifa zote za nchi kwa rais mteule.

Tags