Jun 18, 2021 08:18 UTC
  • Rais Hassan Rouhani
    Rais Hassan Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo baada na kupiga kura yake katika uchaguzi wa Rais amesema kuwa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ni miongoni mwa chaguzi muhimu sana hapa nchini na kwamba dunia nzima inafuatilia uchaguzi huo.

Rais Rouhani mesema kuwa, wananchi wa Iran wanaelewa vyema  umuhimu wa uchaguzi wa leo katika mustakbali wao na Jamhuri ya Kiislamu. Amewataka wananchi kufumbia macho masuala yote ya kabla ya uchaguzi wa leo na kuhudhuria kwa wingi katika zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kumchagua mgombea wao. 

Ameashiria jinsi uchaguzi wa rais hapa nchini unavyofanyika kwa wakati na bila ya kuahirishwa hata mara moja na kusema, ripoti iliyowasilishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani inaonesha kuwa, hakujaripotiwa hata kisa kimoja cha ghasia au ukosefu wa amani katika eneo lolote la Iran hadi hivi sasa. 

Amesema anatarajia kuwa wananahi wa Iran watatekeleza vyema haki na wajibu wao wa kitaifa, kimapinduzi na kidini kwa kushiriki kwa wingi katika zoezi la uchaguzi wa leo. 

Uchaguzi wa rais nchini Iran

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, mamilioni ya Wairani wakiongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei tangu mapema leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kuchagua Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wawakilishi wao katika Mabaraza ya Miji na Vijiji.

Baada ya kupiga kura Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, siku ya uchaguzi ni siku ya taifa na kuongeza kuwa: Leo wananchi ndio wenye uwanja na medani na kwa kura zao wanaainisha ramani ya nchi kwa ajili ya miaka kadhaa ijayo, hivyo leo ni siiku yao.

Tags