Jun 27, 2024 08:08 UTC
  • Barua ya wanazuoni wa Kisunni wa Iran kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu uchaguzi  wa kesho

Katika barua waliyomuandikia Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, zaidi ya wanazuoni elfu mbili wa Kisunni wa Iran wamesema kuwa uchaguzi wa rais utakaofanyika kesho Ijumaa hapa nchini utaimarisha nguvu na irada ya taifa la Iran.

Duru ya 14 ya uchaguzi wa rais wa Iran imepangwa kufanyika katika pembe zote za nchi kesho Ijumaa tarehe Juni 28 ili kumchagua rais wa tisa wa Iran kufuatia ajali ya helikopta iliyopelekea kufa shahidi Ras Ebrahim Raisi kiwa na viongozi wenzake wa kitaifa huko kaskazini magharibi mwa nchi, wakiwa katika safari ya kikazi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, watu elfu mbili na mia sita katika maimamu wa swala za Ijumaa na jamaa, wakurugenzi wa shule za kawaida na za kidini na wanazuoni wa Kisunni wa Iran wamemwandikia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambapo huku wakirejelea kusisitiza mapatano, utiifu na imani zao kwa malengo matukufu ya Imam Khomeini (MA), mashahidi watukufu na pia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, wamesema kwamba upigaji kura ni haki na wajibu usioweza kubatilishwa wa kila Muirani. Wamesisitiza kwamba, kwa yakini uchaguzi ujao utaimarisha msingi wa nguvu na irada ya taifa pamoja na kuandaa uwanja wa mustakbali na kesho yenye fahari kwa Wairani wote, wakiwemo Waajemi, Wakurdi, Waturuki, Wabaluchi, Waturkmeni, Walori, Shia na Sunni na wafuasi wa dini zote za mbinguni.

Barua hii imeandikwa na kutiwa saini na wanazuoni wa Kisunni kutoka mikoa ya Kermanshah, Hormuzgan, Khorasan Rizvi, Khorasan Kusini, Khorasan Kaskazini, Bushehr, Fars, Kurdistan, Golestan, Sistan na Balochistan, Azabajani Magharibi na Gilan.

Tags