Jun 28, 2024 07:19 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Watu hawapaswi kuwa na shaka yoyote kuhusu kushiriki katika uchaguzi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka wananchi wa Iran kutosita hata kidogo kushiriki katika uchaguzi wa leo wa Rais.

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepiga kura yake katika sanduku la kupigia kura leo Ijumaa asubuhi wakati wa kuanza zoezi la upigajii kura wa duru ya 14 ya uchaguzi wa Rais, ambapo amepiga kuura yake katika kituo cha kupigia kura cha Husseiniya ya Imam Khomeini.

Baada ya kupiga kura yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja siku ya uchaguzi kuwa siku ya furaha na nishati kwa Wairani na kuashiria uthabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia ushiriki wa wananchi katika uchaguzi. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: Wananchi wapendwa wa Iran, suala la kupiga kura na kushiriki katika mtihani huu muhimu wa kisiasa lichukulieni kwa uzito jambo hili na msiruhusu hali yoyote ya shaka na kusitasita iingie katika nafsi zenu.

Muhammad Mokhber, Kaimu Rais wa Iran akipiga kura

 

Ayatullah Khamenei ameutambua ushiriki wa wananchi kwa shauku na hamasa katika uchaguzi na wingi wa wapiga kura kuwa ni hitajio la uhakika kwa Jamhuri ya Kiislamu na akasema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama jina lake linavyojieleza, uwepo na mahudhurio ya watu ni jambo linalozingatiwa katika dhati yake na kwa msingi huo, hadhi na heshima ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran duniani inategemea  mahudhurio ya watu.

Wagombea wanne wanachuana kuwania kiti cha Urais ambao ni Saeed Jalili, mkuu wa zamani wa timu ya mazungumzo ya nyuklia, Muhammad Bagher Qalibaf, spika wa Bunge la Iran, Mostafa Pourmohammadi, waziri wa zamani wa mambo ya ndani na Masoud Pezeshkian, waziri wa zamani wa afya.

Tags