Jun 30, 2024 02:14 UTC
  • Sayyid Nasrullah: Kukombolewa Palestina ndio ushindi wa mwisho

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, ushindi wa mwisho ni kukombolewa Palestina na kuondolewa eneo la Asia Magharibi kutoka katika udhibiti utawala wa Marekani.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo katika risala yake katika Kongamano la Kimataifa la Mashahidi wa Muqawama na Walinzi wa Haram na kuongeza kuwa: Uungaji mkono na mapambano ya wananchi yametuweka kwenye njia ya kupata ushindi mkubwa na wa mwisho ambao ni kukombolewa Palestina kutoka katika satwa ya Wazayuni na kukombolewa eneo zima kutoka katika udhibiti wa utawala wa Marekani.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema wa ushindi huu wa mwisho unahitaji juhudi na jihadi yenye kuendelea bila kuchoka na akasema: Ni lazima kuwa na imani kamili na yakini katika ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba waumini wakwe watashinda.

Ayatullah Ali Khamenei akizungumza na wajumbe wa Kongamano la Kimataifa la Mashahidi wa Muqawama na Walinzi wa Haram 

 

Akigusia jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kuuawa shahidi maelfu ya watu ambao wengi wao ni watoto na wanawake, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa: Leo hii wananchi wetu katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na uhajiri, njaa, na njaa, mzingiro na mauaji ya halaiki, na kambi za muqawama hususan Lebanon, Yemen na Iraq zinawasaidia.

Kongamano la Kimataifa la Mashahidi wa Muqawama na Walinzi wa Haram  lilianza jana Jumamosi katika Haram ya imam Ridhja (as) katika mji wa Mash'had likihudhuriwa na familia za mashahidi Walinzi wa Haram kutoka nchi 7.

Tags