Jun 29, 2024 02:56 UTC
  • Matokeo ya awali yaanza kutolewa Iran baada ya saa 16 za kupiga kura katika uchaguzi wa Rais

Msemaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Iran ametangaza matokeo mapya ya uchaguzi wa jana wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ambao ulifanyika kwa muda wa saa 16 baada ya kuongezewa muda mara kadhaa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Mohsen Eslami, Msemaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Iran amesema kuwa, matokeo mapya na rasmi yaliyoifikia tume hiyo hadi wakati anatoa taarifa hiyo ilikuwa ni kura milioni 12,058,843 zikiwemo zilizoharibika. 

Idadi ya kura hizo kwa mujibu wa wagombea ni kama ifuatavyo: 

Pezeshkian: Kura 5,000,354.

Jalili: Kura 4,875,269.

Ghalibaf: Kura 1,620,628

Pour Mohammadi: Kura 95,172

Upigaji kura katika uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulianza saa mbili asubuhi jana Ijumaa, tarehe 28 Juni 2024 katika vituo 58,640 vya kupigia kura kote nchini. 

Idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa kubwa kiasi kwamba zoezi hilo limeongezewa muda mara kadhaa. Wataalamu wa mambo walitabiri mapema kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa zoezi hilo kuingia katika duru ya pili.