Jul 01, 2024 07:02 UTC
  • Hamas: Kitendo cha Israel cha kuwatumia mateka kama ngao za binadamu ni uhalifu wa kivita

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas); Izzat al-Rashq amesema kuwa, hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuwatumia mateka kama ngao za binadamu ni jinai ya kivita.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la IRNA; Izzat al-Rashq", amesema hayo na kusisitiza kuwa, hatua ya wanajeshi wa Israel ya kuwatumia mateka wa Kipalestina kama ngao za binadamu wakati wa operesheni zao za kigaidi katika Ukanda wa Gaza ni uhalifu kwa maana halisi ya neno na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za vita na haki za binadamu.

Mjumbe huyo wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS ameongeza kuwa: jinai nyingine zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya mateka wa Palestina katika korokoro za kinazi na Kizayuni, ni pamoja na kuwatesa kwa njaa, udhalilishaji na mateso mengine mengi, kupuuza matibabu kwa makusudi, kunyimwa dawa, kuvunjwa mikono na miguu, kuwanyonga na kuwapa adhabu ya mauaji ya hatua kwa hatua.

Wanajeshi makatili wa Israel wanafanya jinai kubwa dhidi ya watoto wadogo mbele ya kimya cha kutisha cha madola ya kibeberu na vibaraka wao. 

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa HAMAS ameitaka Jamii ya Kimataifa, Mahakama ya Kimataifa ya Haki(ICJ) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuchukkua hatua kali dhidi ya utawala wa Kizayuni. 

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Wapalestina 37, 877 wameshauawa shahidi na wengine 86,969 wameshajeruhiwa tangu Israel ilipoanzisha vita vya kinyama na kikatili dhidi ya watu wa Ghaza huko Palestina, tarehe 7 Oktoba, 2023. 

Tags