Jun 28, 2024 09:17 UTC
  • HRW yakosoa kucheleweshwa kutiwa mbaroni Benjamin Netanyahu

Mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch kwa barani Ulaya ameikosoa mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kuchelewa kumtia mbaroni waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu kwa jinai zake za kutisha dhidi ya Wapalestina.

Shirika la habari la SAMA la Palestina limeripoti habari hiyo na kumnukuu Rami Abdu, Mkuu wa Human Rights Watch barani Ulaya na Mediterania akiilaumu vikali mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kuendelea kumwangalia kwa macho tu nduli wa Israel, Banjemin Netanyahu na waziri wake wa vita, Yoav Gallant wakati wanaendelea kufanya jinai mbaya sana za kivita huko Ghaza.

Amesema: Hukumu ya mwisho iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ni aina fulani ya kuruhusu kuendlea jinai dhidi ya wananchi wa Ghaza.

Rami Abdu, Mkuu wa Human Rights Watch barani Ulaya na Mediterania

 

Katika upande mwingine, gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth lilikuwa limetabiri kwamba tarehe 24 Julai yaani kabla ya safari ya Netanyahu huko Marekani, mahakama ya ICC itakuwa imeshatoa amri wa kutiwa mbaroni waziri mkuu huyo wa utawala wa Israel na waziri wake wa vita.

Iwapo matamshi ya gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth yatakuwa ni kweli, na kama mahakama ya ICC itatoa waranti wa kutiwa mbaroni nduli hao wa Israel, basi Netanyahu na Gallant watapigwa marufuku kutembelea nchi 124 duniani.

Nduli wawili wa Israel wanaosakwa kwa jinai zao za kivita, Netanyahu na Gallant

 

Lakini cha kusikitisha ni kuwa, licha ya kupita karibu miezi 9 ya jinai za kutisha mno zinazofanywa na Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ghaza huko Palestina, hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa na jamii ya kimtaifa za kujaribu kuzuia jinai hizo ambazo ni mara chache zimetokea au hazijawahi kutokea mfano wake katika historia ya mwanadamu.