Jun 30, 2024 11:19 UTC
  • Azma ya Iran na Libya ya kuimarisha uhusiano mzuri wa zamani

Katika hafla ya kuwasilisha nyaraka zake za utambulisho kwa Mkuu wa Baraza la Rais la Libya, balozi mpya wa Jamjuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza utayarifu wa Iran wa kurejesha haraka uhusiano mzuri wa zamani uliokuwepo kati ya nchi mbili hizi za Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Jumamosi, Shirika la Habari la ISNA limesema kuwa Ainullah Suri, balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Libya, alikutana na Mohammed Al-Manfi, Mkuu wa Baraza la Rais la Libya, na kumkabidhi hati zake za utambulisho mwanzoni mwa kazi yake kama balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Libya.

Katika mazungumzo hayo, Suri, ameorodhesha nyanja nyingi za ushirikiano wa pamoja kati ya nchi mbili, zikiwemo fursa za kibiashara, kiuchumi na hasa kiufundi na uhandisi, afya, dawa, matibabu na elimu ya juu, na kusisitiza kuwa ufuatiliaji wa viongozi wa ngazi za juu wa nchi mbili utakuwa na mchango mkubwa katika kutumika vizuri suhula zilizopo katika nyama hizo kwa manufaa ya watu wa mataifa mawili haya.

Katika mazungumzo hayo, Mkuu wa Baraza la Rais la Libya amesisitiza utayarifu wa Libya wa kupanua uhusiano wa nchi mbili na kuongeza kuwa nchi hiyo ya Afrika iko tayari kubadilishana wajumbe wa ngazi za juu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.