-
Iran: Mapatano ya JCPOA hayawezi kujadiliwa upya
Mar 04, 2021 08:37Mapatano ya nyuklia ya JCPOA hayawezi kujadiliwa upya na njia pekee ya kuyalinda na kuyahuisha ni Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.
-
Tehran: Vikwazo vya Marekani vimekiuka haki za raia wa Iran
Mar 04, 2021 03:25Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa vikwazo vya upande mmoja, haramu na vya kidhalimu vya Marekani vimekiuka haki za taifa la Iran na nchi hiyo haina haki ya kuzungumzia au kuwa na wasiwasi kuhusu haki za binadamu nchini Iran.
-
Kiongozi Muadhamu amuomboleza mwanazuoni wa Kiislamu Lebanon, Sheikh Ahmed al-Zein
Mar 04, 2021 01:18Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemtumia ujumbe wa rambirambi Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon kufuatia kuaga dunia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Maulamaa Waislamu Lebanon.
-
Iran: Wamarekani wawajibike kuhusu jinai wanazofanya huko Yemen, waache bwabwaje
Mar 04, 2021 00:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema kuwa Wamarekani wanapaswa kuwajibika kutokana na jinai na uhalifu wao wa miaka 6 sasa huko Yemen badala ya kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya nchi nyingine.
-
Rais Rouhani: Mapatano ya JCPOA hayalindiki kwa kaulimbiu na maneno, yanahitaji vitendo
Mar 03, 2021 10:20Rais Hassan Rouhani amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasubiri kuona hatua za kivitendo kuhusiana na makubaliano ya nyuklia na akasisitiza kuwa makubaliano hayo ya JCPOA hayalindiki kwa kaulimbiu na maneno matupu.
-
Rouhani: Makubaliano ya JCPOA hayajadiliki tena, njia pekee ya kuyalinda ni kuondolewa vikwazo vya Marekani
Mar 03, 2021 00:53Rais Hassan Rouhani amesema, JCPOA ni makubaliano ya kimataifa ya pande kadhaa zinazojulikana wazi na yamethibitishwa na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na akasisitiza kwamba, makubaliano hayo ya nyuklia hayawezi katu kujadiliwa tena na njia pekee ya kuyalinda na kuyafufua ni kuondolewa vikwazo vya Marekani.
-
Mtazamo wa Iran kuhusu matukio ya Yemen; kuangazia viini vya jiostratijia katika eneo la Asia Magharibi
Mar 03, 2021 00:25Ismail Baqai Hamaneh, mwakilishi wa kudumu wa Iran katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneza Uswisi amesema kuwa, wale ambao wanapiga ngoma ya vita, wanapaswa kusitisha uuzaji silaha ambazo kimsingi zinatumika kwa ajili ya kuwauwa wananchi wasio na hatia.
-
Msemaji wa Serikali ya Iran: Marekani haina njia nyengine ghairi ya kurejea katika mapatano ya JCPOA
Mar 02, 2021 08:55Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu zimefeli na Marekani haina njia nyingine ghairi ya kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Rouhani: Marekani haina budi ila kuipigia Iran magoti
Mar 01, 2021 23:17Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kukiri serikali ya Marekani kuhusu kufeli mashinikizo na vikwazo vyake dhidi ya Iran ni mafanikio makubwa kwa taifa la Iran.
-
Zarif: Marekani haina haki ya kurejea JCPOA hadi pale itakapotekeleza majukumu yake
Mar 01, 2021 23:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema Marekani haina haki ya kurejea katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hadi pale itakapotekeleza majukumu yake.