-
Khatibzadeh: Tuhuma na vitisho dhidi ya Iran havisaidii chochote
Mar 01, 2021 09:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa kutoa tuhuma na kuitishia Iran hakutasaidia chcochote na kuongeza kuwa Iran itatoa jibu chanya kwa hatua chanya.
-
Jibu la Iran kwa pendekezo la “Josep Borrell” la kufanyika kikao kisicho rasmi cha JCPOA
Mar 01, 2021 08:00“Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona kuwa huu si wakati mwafaka wa kufanyika kikao kisicho rasmi kilichopendekezwa na Mkuu wa Sera za Kigeni za Umoja wa Ulaya baina ya nchi hizo na Tehran kuhusu kadhia ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.”
-
Iran: Tutaendelea kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina
Mar 01, 2021 03:21Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Qatar jana alionana na Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Doha na kusisitiza kuwa Tehran itaendelea kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.
-
Iran yazipongeza Pakistan na India kwa kulinda usimamishaji vita
Mar 01, 2021 03:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Tehran inazipongeza Pakistan na India kwa tamko lao la pamoja la kuyalinda makubaliano ya kusimamisha vita na kusema kuwa hiyo ni hatua nzuri ya kuelekea kwenye amani na utulivu wa kudunu katika eneo la kusini mwa Asia.
-
Khatibzadeh: Huu si wakati mwafaka wa kuitishwa kikao cha JCPOA
Feb 28, 2021 23:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, kwa kutilia maanani misimamo na hatua za karibuni za nchi tatu za Ulaya na Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona kuwa huu si wakati mwafaka wa kufanyika kikao kisicho rasmi kilichopendekezwa na Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya baina ya nchi hizo na Tehran kuhusu kadhia ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran yapokea dozi robo milioni za chanjo ya Corona kutoka China
Feb 28, 2021 09:51Shehena ya kwanza ya dozi za chanjo ya kubaliana na ugonjwa wa Covid-19 kutoka China imewasili hapa nchini Iran leo Jumapili.
-
Shamkhani: Iran haitaruhusu kuhuishwa ugaidi wa kitakfiri katika eneo
Feb 27, 2021 08:58Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na mataifa mengine yanayopambana na ugaidi katu hayataruhusu kuhuishwa magenge ya kigaidi na kitakfiri katika eneo la Asia Magharibi.
-
Iran: Vikwazo visipoondolewa katika miezi 3 ijayo tutaondoa kamera za ukaguzi za IAEA
Feb 27, 2021 03:50Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (AEOI) amesema kuhusu mapatano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kwamba, kwa muda wa miezi mitatu, IAEA haitakuwa na haki ya kuangalia kamera na mifumo ya kurekodia taarifa; na kama vikwazo havitaondolewa katika miezi mitatu ijayo, taarifa hizo zitafutwa na kamera za wakala huo wa nishati ya atomiki zitaondolewa.
-
Wairani wataka makubaliano ya nyuklia yatekelezwe kikamilifu kabla ya kufanya mazungumzo na Marekani
Feb 26, 2021 23:50Uchunguzi wa maoni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Maryland kikishirikiana na taasisi ya Canada ya Iran Poll umeonyesha kuwa, asilimia kubwa ya Wairani wanaamini kuwa Tehran haipasi kufanya mazungumzo na Marekani kabla ya nchi hiyo kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Namaki: Iran inakaribia kuwa kitovu kikuu cha uzalishaji na uuzaji nje chanjo
Feb 26, 2021 10:03Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran ametangaza kuwa: Hadi kufikia msimu ujao wa machipuo Iran itakuwa moja ya kambi kubwa za kuzalisha na kuunza nje chanjo duniani.