Khatibzadeh: Tuhuma na vitisho dhidi ya Iran havisaidii chochote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67404-khatibzadeh_tuhuma_na_vitisho_dhidi_ya_iran_havisaidii_chochote
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa kutoa tuhuma na kuitishia Iran hakutasaidia chcochote na kuongeza kuwa Iran itatoa jibu chanya kwa hatua chanya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 01, 2021 09:09 UTC
  • Khatibzadeh: Tuhuma na vitisho dhidi ya Iran havisaidii chochote

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa kutoa tuhuma na kuitishia Iran hakutasaidia chcochote na kuongeza kuwa Iran itatoa jibu chanya kwa hatua chanya.

Saeed Khatibzadeh leo amezungumza na waandishi wa habari na kuashiria mtazamo wa Iran kuhusu pendekezo lililotolewa na Josep Borrell Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya kwa ajii ya kufanyika kikao cha pamoja na Marekani na Ulaya na kubainisha kuwa: Tumesema kuwa msimamo wa Iran uko wazi na thabiti na hakuna jambo litakalobadilika katika uwanja huo. 

Khatibzadeh amesema kuwa, njia pekee ya Marekani ni kujitoa katika siasa za makosa za serikali iliyopita; lakini kwamba kufikia sasa hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika katika siasa hizo zilizo na za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, iwapo Marekani inataka kuwa na nafasi katika meza ya JCPOA basi inapasa kurejea katika mapatano hayo na kisha itekeleza ahadi na majukumu yake na kundoa vikwazo. 

Mapatano ya JCPOA yaliyopasishwa na Baraza la Usalama la UN 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezihutubu pia pande za Ulaya katika mapatano ya JCPOA na kueleza kuwa,  njia ya kushirikiana ni njia bora kuliko njia nyingine zozote; kwa sababu kitendo cha kutoa tuhuma na vitisho dhidi ya Iran hakisaidii lolote na Iran inatoa jibu chanya kwa ushirikiano inaopatiwa na upande wa pili. 

Kuhusu uwezekano wa kupasishwa azimio dhidi ya Iran katika Bodi ya Magavana ya wakala wa IAEA na kusitishwa ushirikiano kati yake na IAEA, Saeed Khatibzadeh amesema: Serikali ya Biden imekuwa na mwanzo wa kukatisha tamaa katika kutekeleza majukumu yake na njia ya kushirikiana Iran na wakala wa IAEA iko wazi kabisa.