-
Araghchi na Guterres wajadili migogoro ya Gaza, Yemen
Oct 21, 2025 08:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres wamefanya mazungumzo ya simu na kuzungumzia matukio ya kikanda ikiwemo hali ya Gaza na Yemen.
-
Iraq: Hatutaruhusu ardhi na anga yetu zitumike kutishia usalama wa Iran, majirani wengine
Oct 21, 2025 03:31Iraq iimesisitiza kuwa haitaruhusu ardhi na anga yake zitumike kutishia usalama wa Iran au wa nchi nyingine yoyote jirani.
-
Kamanda wa Iran: Miundomsingi ya makombora haikupata 'hata mkwaruzo' wakati wa Vita vya Siku 12
Oct 20, 2025 23:53Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, miundomsingi ya makombora na ulinzi imebaki imara kama ilivyokuwa kabla ya Vita vya Siku 12 na kubainisha kwa kusema: "mkwaruzo wenye ukubwa hata wa ubawa wa nzi" haukufanywa kwenye makombora ya Iran.
-
Imamu Khamenei amwambia Trump: Badala ya kuingilia mambo ya nchi zingine, tuliza maandamano ya mamilioni ya wananchi dhidi yako
Oct 20, 2025 09:34Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali matamshi ya hivi karibuni ya Rais Donald wa Marekani kuhusu Iran na eneo la Asia ya Magharibi na na kusema, Trump alisafiri hadi Palestina iliyokaliwa kwa mabavu na kutoa maneno matupu yenye kejeli ili kuwatia moyo Wazayuni waliokata tamaa.
-
Meja Jenerali Pakpour: Iran iko tayari kikamilifu kuimarisha uhusiano wa kistratejia na Yemen
Oct 20, 2025 03:14Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limesema kuwa limejiandaa kikamilifu kukuza ushirikiano wa kimkakati na vikosi vya ulinzi vya Yemen katika mapambano dhidi ya mabeberu wa dunia na Uzayuni wa kimataifa.
-
Iran yalaani kitendo cha Israel cha kumtesa mwanaharakati Greta Thunberg
Oct 20, 2025 03:13Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumtesa mwanaharakti wa haki za binadamu aliyedhihirisha mshikamano na watu wa Palestina. Baqaei amevitaja vitendo hivyo vya Israel kuwa vya ukatili, visivyo vya kibinadamu na vya udhalilishaji.
-
Jan Eliasson: Kurudishwa vikwazo dhidi ya Iran ni hatua ya kurudi nyuma
Oct 19, 2025 07:55Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Uswidi amesisitiza kwamba Troika ya Ulaya imetokomeza uwezo wake wa kuwa na nafasi huru katika eneo la Asia Magharibi kwa kurejesha vikwazo dhidi ya Iran.
-
Iran yailaani Israel kwa kuendelea kuua wanawake na watoto Gaza
Oct 19, 2025 03:10Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baghaei amelaani ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel, likiwemo shambulio la hivi karibuni dhidi ya gari lililokuwa limebeba familia ya Kipalestina wakati ikirejea kwenye makazi yao.
-
Iran yazindua makombora ya Emad, Ghadr yaliyoboreshwa
Oct 19, 2025 03:06Kikosi cha Wanaanga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimezindua makombora yaliyoboreshwa ya Emad na Ghadr katika miji ya makombora ya chini ya ardhi.
-
Barua ya Araqchi kwa Guterres na Baraza la Usalama: Muda wa azimio 2231 umemalizika
Oct 18, 2025 09:26Seyyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema katika barua rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mwenyekiti wa Kiduru wa Baraza la Usalama Vassily Nebenzia kwamba muda wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama unamalizika leo tarehe 18 Oktoba 2025.