Iran kuokoa dola milioni 30 kwa kujizalishia aina 63 za dawa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136404-iran_kuokoa_dola_milioni_30_kwa_kujizalishia_aina_63_za_dawa
Iran imezindua bidhaa mpya 63 za dawa zinazozalishwa ndani ya nchi—ikiwa ni pamoja na fomula 19 zinazozalishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini—hatua inayotarajiwa kuifanya nchi hiyi iokoe kati ya dola milioni 25 na 30 kila mwaka kwa fedha muhimu za kigeni, kwa kupunguza utegemezi wa dawa na malighafi zinazoagizwa kutoka nje.
(last modified 2026-02-08T09:14:09+00:00 )
Feb 08, 2026 09:14 UTC
  • Iran kuokoa dola milioni 30 kwa kujizalishia aina 63 za dawa

Iran imezindua bidhaa mpya 63 za dawa zinazozalishwa ndani ya nchi—ikiwa ni pamoja na fomula 19 zinazozalishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini—hatua inayotarajiwa kuifanya nchi hiyi iokoe kati ya dola milioni 25 na 30 kila mwaka kwa fedha muhimu za kigeni, kwa kupunguza utegemezi wa dawa na malighafi zinazoagizwa kutoka nje.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa dawa hizo hapa Tehran, Mohammad Naderi Alizadeh amesema leo Jumapili kwamba, Kampuni ya Uwekezaji wa Dawa ya Tamin (TIPICO) ya Iran ni mojawapo ya makampuni machache nchini ambayo yanadhibiti mnyororo mzima wa thamani ya dawa, kuanzia uzalishaji wa utafiti na maendeleo, hadi utengenezaji, usambazaji, na uuzaji.

Amesema shirika hilo linaendesha matawi 24 na makampuni matatu tanzu nchini kote na huzlisha bidhaa 549 za dawa, zinazokidhi mahitaji mengi ya matibabu nchini Iran.

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo inashikilia 25-30% ya soko la usambazaji wa dawa nchini Iran na hutoa dawa kwa zaidi ya 40% ya Vyuo Vikuu vya Tiba (Udaktari), vingi vikihudumia idadi ya watu wenye kipato cha chini.

Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji huyo, TIPICO imeondoa matawi yote yanayopata hasara na kuboresha utendaji wa kifedha kwa kiasi kikubwa.

Faida ya jumla ya kampuni zake iliongezeka kwa 138% katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka huu wa Kiirani (Machi 21, 2025 hadi Januari 20, 2026), huku jumla ya faida ya kikundi ikiongezeka maradufu.

Mapema mwezi uliopita, Mkurugenzi wa utafiti na maendeleo wa kampuni inayotegemea maarifa nchini Iran alitangaza habari ya uzalishaji wa dawa ya 'Ofenib' kwa mara ya kwanza hapa nchini, ambayo hutumika kwa watu wenye magonjwa ya mapafu ya ndani, hasa fibrosis ya mapafu.