-
Februari 23 Iran itajitoa katika utekelezaji wa hiari wa Itifaki ya Nyongeza ya NPT
Jan 28, 2021 04:25Mkuu wa kamati ya usalama wa taifa na sera za nje ya Bunge la Iran amesema, tarehe 23 ya mwezi ujao wa Februari Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itajitoa katika utekelezaji wa hiari wa Itifaki ya Nyongeza (Additional Protocol) ya mkataba unaopiga marufuku uundaji na uenezaji silaha za nyuklia NPT.
-
Iran yazindua 'Jumba la Ubunifu na Teknolojia' Nairobi, Kenya
Jan 28, 2021 00:50Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuzinduliwa Kituo cha Ubunifu na Teknolojia cha Iran (IHIT) katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Iran na Kenya na hata nchi nyingine za kanda ya Afrika Mashariki.
-
Vaezi: Israel haina nguvu za kijeshi za kutoa pigo kwa Iran
Jan 28, 2021 00:47Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel hauna mpango, uwezo, nguvu wala mkakati wa kulishambulia kijeshi taifa hili.
-
Faili jeusi la Ulaya la kuupatia silaha za kemikali utawala wa Saddam katika vita vya miaka 8 dhidi ya Iran
Jan 27, 2021 23:05‘Kupita kwa muda hakusahaulishi uovu, wala hakusafishi uchafu wa jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu za utumiaji wa silaha za kemikali.’
-
Rouhani: Ulaya haijatekeleza ahadi zake; ikirejea katika majukumu yake nasi pia tutarejea
Jan 27, 2021 08:50Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran itarejea katika mapatano ya JCPOA kwa sharti kwamba Marekani na Ulaya nazo zitekeleze majukumu yao.
-
Watu 2 wauawa katika tukio la utekaji nyara jimboni Texas, Marekani
Jan 27, 2021 08:37Watekajinyara wamewaua watu wawili katika jimbo la Texas, Marekani.
-
Gavana wa Benki Kuu: Oman ni mshirika wa kistratejia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jan 27, 2021 04:32Gavana wa Benki Kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Oman ni mshirika wa kistratejia wa Tehran; kwani licha ya mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani, lakini taifa hilo limeendelea kuwa na uhusiano wake wa Kibenki na Tehran
-
Takht Ravanchi: Utapeli ndio msingi mkuu wa siasa za mambo ya nje za Israel
Jan 27, 2021 00:59Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, utapeli na kujionesha kuwa ni watu waliodhulumiwa, ndio msingi mkuu wa siasa za mambo ya nje za utawala wa Kizayuni akisisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina haki ya kujihami mbele ya vitisho vya utawala huo pandikizi.
-
Zarif: Iran iko tayari kushirikiana na Russia kuhusu maeneo ya Caucasia na Ghuba ya Uajemi
Jan 27, 2021 00:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushirikiano wa Iran na Russia ni kwa ajili ya amani na uthabiti katika eneo. Ameongeza kuwa: "Tuko tayari kushirkiana na Russia katika masuala ya Caucasia na Ghuba ya Uajemi."
-
Amir Abdolahian: Uhusiano wa Iran, China na Russia ni wa kiistratijia
Jan 26, 2021 07:40Mshauri Mkuu wa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, uhusiano wa Tehran, Beijing na Moscow ni wa kiistratijia na kuongeza kuwa, uhusiano na nchi za dunia ambazo zilikuwa pamoja na wananchi wa Iran wakati wa hali ngumu umejengeka juu ya msingi na stratijia ya urafiki, ushirikiano na kuheshimiana.