-
Namaki: Uwekaji vikwazo visivyo vya kisheria wakati wa janga la maradhi ni kielelezo cha mauaji ya kimbari
Oct 12, 2020 23:14Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema, uwekaji vikwazo visivyo vya kisheria na uchukuaji hatua za mabavu hususan wakati wa janga la maradhi yaliyoikumba dunia nzima ni kielelezo cha mauaji ya kimbari.
-
Khatibzadeh: Vikwazo vya silaha dhidi ya Iran vitaondolewa tarehe 18 Oktoba
Oct 12, 2020 23:11Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran unatarajiwa kumalizika usiku wa tarehe 18 mwezi huu.
-
Zaidi ya wagonjwa 4,000 wapya wa corona wagunduliwa Iran; vifo vipya 272 vyaripotiwa
Oct 12, 2020 09:59Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa wapya elfu nne (4,000) wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini katika kipindi cha saa 24 zlizopita.
-
Malengo ya Marekani ya kushadidisha vikwazo dhidi ya Iran; kwa mtazamo wa Waziri wa Ulinzi
Oct 12, 2020 07:38Sambamba na kuvunja vibaya maazimio na sheria za kimataifa, Marekani imeamua pia kuwawekea wananchi wa Iran vikwazo vya kidhalimu na inaendesha vita vya pande zote vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo kubwa la Kiislamu.
-
Amiri Jeshi Mkuu: 'Wahuni wapayukaji' nchini Marekani wana kiwewe na uwezo wa Iran
Oct 12, 2020 10:02Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sababu ya makelele na bwabwaja za wahuni wapayukaji nchini Marekani kuhusiana na uwezo wa kiulinzi, makombora na kieneo wa Iran ni kwamba, wahusika wametambua mahesabu makini na ya kiakili ya taifa hili kwa ajili ya kufikia uwezo huu.
-
Khatibzadeh: Watawala wa Marekani wamepata pigo la kihistoria mkabala na Iran
Oct 11, 2020 23:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa watawala wa Marekani wamepata pigo la kihistoria mbele ya Iran na kusisitiza kuwa, muda si mrefu viongozi hao wa Marekani watakiri rasmi kushindwa kwao.
-
Iran: Marekani ni kidhabi kwa kudai vikwazo vipya havilengi sekta ya afya
Oct 11, 2020 08:41Waziri wa Afya wa Iran amelaani hatua ya Marekani ya kuliwekea vikwazo shadidi taifa hili na kubainisha kuwa, utawala wa Washington umekubuhu kwa kusema uwongo, kwa madai yake kuwa vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu havilengi sekta ya afya na tiba.
-
Trump anaitusi Iran kwa sababu amefeli katika njama zake dhidi ya Iran
Oct 11, 2020 04:31Mwenyekiti wa Baraza la Kistratijia la Sera za Kigeni la Iran, Dkt. Kammal Kharrazi, ametoa kauli kufuatia matamshi yaliyojaa matusi ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusema, Trump amepandwa na hasira baada ya kufeli njama zake dhidi ya Iran.
-
Marais wa Iran na Russia waelezea wasiwasi wao kuhusu vita vya Nagorno-Karabakh
Oct 11, 2020 00:47Marais wa Iran na Russia wameelezea wasiwasi wao kutokana na kuendelea mgogoro wa Nagorno-Karabakh na wamesema wana hofu mgogoro huo usije ukageuka kuwa vita vya eneo hili zima kutokana na uingiliaji wa nchi nyingine na kuweko magenge ya kigaidi katika eneo hilo.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China washauriana kuhusu ushirikiano wa kiistratijia
Oct 11, 2020 00:44Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China wamefanya mashauriano ya pamoja kuhusu Mpango Mkuu wa Ushirikiano wa Kiistratijia wa nchi mbili.