Trump anaitusi Iran kwa sababu amefeli katika njama zake dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63950-trump_anaitusi_iran_kwa_sababu_amefeli_katika_njama_zake_dhidi_ya_iran
Mwenyekiti wa Baraza la Kistratijia la Sera za Kigeni la Iran, Dkt. Kammal Kharrazi, ametoa kauli kufuatia matamshi yaliyojaa matusi ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusema, Trump amepandwa na hasira baada ya kufeli njama zake dhidi ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2020 04:31 UTC
  • Trump anaitusi Iran kwa sababu amefeli katika njama zake dhidi ya Iran

Mwenyekiti wa Baraza la Kistratijia la Sera za Kigeni la Iran, Dkt. Kammal Kharrazi, ametoa kauli kufuatia matamshi yaliyojaa matusi ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusema, Trump amepandwa na hasira baada ya kufeli njama zake dhidi ya Iran.

Kharrazi amesema matusi ya hivi karibuni ya Trump yameonyesha kina cha ukatili wake na kuongeza kuwa matamshi kama hayo si tu kuwa hayataisaidia Marekani kufikia malengo yake bali yatazidi kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Wairani.

Kuhusu vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya benki 18 za Iran, Kharrazi amesema Marekani inalenga kuipigisha magoti Iran kwa vikwazo hivyo vipya lakini kwa mara nyingine itagonga mwamba.

Mwenyekiti wa Baraza la Kistratijia la Sera za Kigeni Iran, Dkt. Kammal Kharrazi

Katika mahojiano ya redio siku ya Ijumaa, rais wa Marekani alikariri madai yake yasiyo na msingi dhidi ya Iran na huku akitumia lugha ya matusi, alidai kuwa utawala wake umetoa onyo kali kwa Iran isichukue hatua yoyote dhidi ya Marekani. 

Weledi wa mambo ya kisiasa nchini Marekani wamemkosoa vikali Trump kwa matamshi yake hayo yaliyojaa matusi dhidi ya Iran.