-
"Israel haiaminiki; Iran inaunga mkono kusimamishwa mauaji ya kimbari Gaza"
Oct 11, 2025 23:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inakaribisha kusitishwa kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza, huku akitoa indhari juu ya tabia ya kutokuwa na muamana Tel Aviv kwa kukiuka makubaliano kadhaa ya huko nyuma.
-
Iran: Tutalinda maslahi yetu Ghuba ya Uajemi hadi tone la mwisho la damu
Oct 11, 2025 02:07Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amegusia uwezekano wa kutokea vita vya moja kwa moja vya kijeshi baina ya Iran na Marekani katika Ghuba ya Uajemi na kusema: Tutajihami na kulinda maslahi yetu katika Ghuba ya Uajemi hadi tone la mwisho la damu.
-
Wananchi wa Iran waandamana; waitaka Israel iheshimu kikamilifu makubaliano ya kusitisha vita Gaza
Oct 10, 2025 23:07Umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tehran na miji mingine kote Iran jana waliandamana kwa lengo la kuiunga mkono Palestina na kuonyesha mshikamano kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Haj Ali Akbari: Israel imepata pigo kubwa miaka miwili baada ya operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa
Oct 10, 2025 08:48Khatibu wa Swala ya Ijumaaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, miaka miwili baada ya Operesheni kubwa ya Kimbunga cha Al-Aqswa haiba ya utawala wa Kizayuni imejaa msukosuko na mparaganyiko.
-
Iran: Maadui wanajua watalazimika ‘kuomba usitishaji vita’ iwapo watatushambulia tena
Oct 10, 2025 03:29Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref amesema matukio ya hivi karibuni yameonyesha nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu na kutangaza kwamba, maadui sasa wanatambua shambulio lolote dhidi ya taifa hili litawalazimu "kuomba kusitishwa kwa mapigano."
-
Iran: Tunaunga mkono mpango wowote wa kumaliza vita, mauaji ya kimbari Gaza
Oct 09, 2025 23:51Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba Jamhuri ya Kiislamu daima inaunga mkono mpango wowote unaolenga kukomesha vita na mauaji ya halaiki huko Gaza, na kusisitiza ulazima wa kuwa macho mkabala wa hulka ya utawala wa Israel ya kukiuka ahadi na makubaliano.
-
Kukabiliana na uchukuaji maamuzi ya upande mmoja; hatua muhimu kwa ajili ya uthabiti wa Asia Magharibi
Oct 09, 2025 09:04Amir-Saeed Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa: "Hali ya eneo la Magharibi mwa Asia ni mbaya mno, na hali hiyo ni matokeo ya uingiliaji kati na siasa za kijeshi za baadhi ya madola ya nje ya eneo, migogoro ya silaha inayoendelea, kukaliwa kwa mabavu kwa muda mrefu na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni."
-
Iran, Russia zajadili kuendeleza ushirikiano wa nyuklia
Oct 09, 2025 03:45Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amekutana na kuzungumza mjini Tehran na afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Taifa la Nishati ya Atomiki la Russia( Russia Rosatom) na kujadili kustawisha ushirikiano katika uga wa nishati ya nyuklia yenye malengo ya amani kati ya nchi mbili hizo waitifaki.
-
IRGC yaonya; Jibu kali litawakabili maadui 'wakikosea' katika Ghuba ya Uajemi, Hormuz
Oct 08, 2025 23:44Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kuwa, hatua zozote za makosa zitakazofanywa na maadui katika Ghuba ya Uajemi, Lango Bahari la Hormuz au katika visiwa vya Iran, zitakabiliwa na jibu kali na la kujutisha.
-
Pezeshkian: Iran ipo tayari kuimarisha uhusiano na Ivory Coast
Oct 08, 2025 09:15Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imejiandaa kikamilifu kupanua ushirikiano wa pande mbili na Ivory Coast ili kufikia malengo ya pamoja.