Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu azuru Haram ya Imam Khomeini (MA)
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136108-kiongozi_wa_mapinduzi_ya_kiislamu_azuru_haram_ya_imam_khomeini_(ma)
Sherehe za kuadhimisha mwaka wa arobaini na saba tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu zimeanza kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuzuru haram haram tukufu ya Imam Khomeini (MA), muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-02-01T02:31:46+00:00 )
Jan 31, 2026 12:56 UTC
  • Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwa katika Haram ya Imam Khomeini (MA)
    Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwa katika Haram ya Imam Khomeini (MA)

Sherehe za kuadhimisha mwaka wa arobaini na saba tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu zimeanza kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuzuru haram haram tukufu ya Imam Khomeini (MA), muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, katika  kumbukumbu ya mwaka wa 47 wa ushindi wa Mapinduzi na mwanzo wa sherehe za 'Afajiri 10', Kiongozi wa Mapinduzi leo asubuhi alifika katika kaburi la Imam Khomeini (rehema za Mungu ziwe juu yake) na kusoma Fatiha kama ishara ya kuheshimu na kuenzi hadhi ya mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei, baada ya kusoma Fatiha na kuswali katika haram ya Imam Khomeini (MA), alimuomba Allah SWT aipe daraja za juu  roho ya Imam huyo mkubwa na mpiganaji wa njia ya haki, pamoja na mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kila mwaka, Wairani na wapenda haki kote duniani huadhimisha kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuanzia tarehe 1 hadi 11 Februari, ambazo hujulikana kama sherehe za Alfajiri Kumi. 

Siku ya kurejea kwa Imam Khomeini nchini Iran (Februari 1) ni mwanzo wa Siku Kumi za Fajr (Siku Kumi za Alfajiri), ambazo hufikia kilele kwa mikusanyiko ya kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 11 Februari.

Taifa la Iran liliupindua utawala wa Pahlavi unaoungwa mkono na Marekani miaka 47 iliyopita, na hivyo kuhitimisha miaka 2,500 ya utawala wa kifalme nchini .

Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na hayati Imam Khomeini yalianzisha mfumo mpya wa kisiasa unaozingatia maadili na demokrasia ya Kiislamu.