Rais Pezeshkian: Trump, Netanyahu, na Ulaya walitaka kuchochea mgawanyiko ndani ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136106-rais_pezeshkian_trump_netanyahu_na_ulaya_walitaka_kuchochea_mgawanyiko_ndani_ya_iran
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na tawala za kigeni, Rais wa Marekani Donald Trump, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na watawala wa Ulaya walijaribu kuchochea vurugu na kuibua mgawanyiko ndani ya Iran.
(last modified 2026-02-01T02:31:16+00:00 )
Jan 31, 2026 12:55 UTC
  • Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian
    Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na tawala za kigeni, Rais wa Marekani Donald Trump, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na watawala wa Ulaya walijaribu kuchochea vurugu na kuibua mgawanyiko ndani ya Iran.

Akizungumza Jumamosi katika haram ya Mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (MA), Rais Pezeshkian amesema kuwa wahusika hao walijaribu taharuki huku wakiunga mkono makundi fulani ambapo baadhi ya watu wasio na hatia walishawishiwa katika hali hiyo na kujikuta wakiwa katika maandamano ya ghasia

Kwa mujibu wa Pezeshkian, lengo lilikuwa kuligawa taifa, kuchochea migogoro na chuki miongoni mwa wananchi, na kuibua mpasuko mkubwa ndani ya jamii.

Waandamanaji wenye silaha na magaidi wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni waliteka nyara maandamano ya amani na ya hapa na pale yaliyohusu malalamiko ya kiuchumi mnamo Januari 8 na 9.

Trump ahamasisha waziwazi matumizi ya vurugu kwa kuwataka waandamanaji wenye silaha kuchukua taasisi za serikali na kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran iwapo magaidi hao wangedhuriwa.

Vurugu hizo ambazo zilichochewa waziwazi na Marekani na utawala wa Israel, zilisababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na binafsi, zikiwemo uharibifu mpana wa maduka, taasisi za serikali, miundombinu ya huduma za umma, pamoja na vifo vya maelfu ya raia na maafisa wa usalama.

Rais wa Iran amebainisha kuwa katika maandamano ya kijamii ya kawaida, watu hawachukui silaha, hawaui wanajeshi, wala kuwasha moto magari ya wagonjwa au masoko. Alisisitiza kuwa serikali ina wajibu wa kusikiliza sauti na malalamiko ya waandamanaji na kushughulikia matatizo yao, akieleza kuwa mamlaka ziko tayari kufanya hivyo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ilikuwa wazi hali hiyo ilizidi maandamano ya kijamii ya kawaida, kwani maadui walitumia changamoto zilizokuwepo kuchochea machafuko na kuendeleza juhudi za kuligawa taifa. Pezeshkian amesisitiza kuwa uwepo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, pamoja na mwongozo wake, umeendelea kuvuruga mipango kama hiyo mara kwa mara na utaendelea kufanya hivyo siku zijazo.