-
Rais Rouhani atuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi: Jeshi ni mlinzi wa roho za Wairani
Apr 17, 2020 08:42Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi ambayo inaadhimishwa leo tarehe 29 mwezi Farvardin na kusisitiza kuwa, jeshi la taifa ni mlinzi wa roho za Wairani katika vita na amani, katika vita laini na ngumu, katika medani ya vita, mitaani, makambini na mahospitalini.
-
"Gwaride la Huduma": Jeshi la Iran liko pamoja na wananchi katika vita dhidi ya corona
Apr 17, 2020 05:05Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima hulinda kiwango cha uwezo wake wa kiulinzi na kumzuia adui kuanzisha mashambulizi na wakati huo huo huwa pamoja na wananchi wakati wa maafa au majanga na kuwasaidia kutatua matatizo yao.
-
Jeshi la Majini la Iran kuunda nyambizi za nyuklia
Apr 17, 2020 00:00Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kikosi hicho kinajiandaa kuunda nyambizi zitakazotumia nishati ya nyuklia zenye uwezo wa kutekeleza operesheni za baharini kwa muda mrefu zaidi katika maji ya kimataifa.
-
Waliopata afueni ya COVID-19 nchini Iran wapindukia elfu 56 huku maambukizo yakiendelea kupungua
Apr 16, 2020 10:41Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, hadi sasa watu 52,229 waliokuwa wameambukizwa kirusi cha COVID-19 hapa nchini wamepata afueni na kuruhusiwa kutoka hospitali.
-
UNDP: Janga la corona linaweza kusambaratisha uchumi wa bara la Afrika
Apr 16, 2020 10:31Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika kanda ya Afrika ametahadharisha kuwa, kuenea kwa virusi vya corona barani Afrika kunaweza kusambaratisha uchumi wa nchi za bara hilo.
-
Kukwepa majukumu katikati ya vita vya corona; Marekani muangamizaji wa roho za watu duniani
Apr 16, 2020 06:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sawa kabisa na wenzo wa "mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa" dhidi ya Iran, kulikatia bila haya Shirika la Afya Duniani WHO vyanzo vya fedha katikati ya janga hili la virusi vya corona kutazidi tu kuichafulia jina nchi hiyo si kitu kingine chochote.
-
Iran: Kitendo cha Marekani cha kuikatia misaada WHO ni jinai dhidi ya binadamu
Apr 16, 2020 03:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya rais wa Marekani ya kulikatia misaada ya kifedha Shirika la Afya Duniani (WHO) tena wakati huu wa mapambano ya dunia nzima dhidi ya corona na kusema kuwa, hatua hiyo ya Marekani ni ushahidi mwingine wa wazi kwamba viongozi wa nchi hiyo ni watenda jinai dhidi ya binadamu.
-
Zarif: Dunia nzima hivi sasa inateseka kwa ubeberu wa Marekani
Apr 15, 2020 20:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea kusikitishwa kwake na uamuzi wa Marekani wa kulikatia misaada Shirika la Afya Duniani (WHO) na kusema kuwa hivi sasa dunia inapita kwenye kipindi cha mateso ya ubeberu wa Marekani.
-
Kwa mara ya kwanza duniani, Iran yavumbua kifaa cha kugundua kilipo kirusi cha corona katika masafa ya mita 100 + Video
Apr 15, 2020 20:13Kwa mara ya kwanza duniani, Jamhuri ya Kislamu ya Iran imevumbua kifaa chenye uwezo wa kugundua mwili na sehemu kilipo kirusi cha corona katika umbali wa mita 100 tena katika kipindi cha sekunde chache tu. Kifaa hicho kimepewa jina la "Musta'an 110."
-
Brigedia Amir Hatami: Jeshi la Iran ni miongoni mwa majeshi yaliyojiweka tayari zaidi duniani
Apr 15, 2020 08:28Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa kuwadia Siku ya Jeshi la Iran amesema kuwa, katika mtazamo wa zana za kijeshi, nguvukazi, mafunzo na mipango, jeshi la nchi hii ni kati ya majeshi yaliyojiweka tayari zaidi duniani.