Brigedia Amir Hatami: Jeshi la Iran ni miongoni mwa majeshi yaliyojiweka tayari zaidi duniani
(last modified Wed, 15 Apr 2020 12:58:35 GMT )
Apr 15, 2020 12:58 UTC
  • Brigedia Amir Hatami: Jeshi la Iran ni miongoni mwa majeshi yaliyojiweka tayari zaidi duniani

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa kuwadia Siku ya Jeshi la Iran amesema kuwa, katika mtazamo wa zana za kijeshi, nguvukazi, mafunzo na mipango, jeshi la nchi hii ni kati ya majeshi yaliyojiweka tayari zaidi duniani.

Inafaa kuashiria kuwa tarehe 29 Farvardin inayosadifiana na tarehe 17 Aprili, nchini Iran na kwa lengo la kuenzi na kuwatunuku askari jasiri wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu, imepewa jina la Siku ya Jeshi. Katika uwanja huo Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Iran leo Jumatano amebainisha kwamba katika kipindi cha miaka 41 iliyopita jeshi la nchi hii limethibitisha utayarifu wake katika medani. Ameongeza kuwa jeshi la Iran linafahamu vyema vitisho, nia na fikra za adui na sambamba na uelewa sahihi wa matukio ya eneo na dunia, limejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana uso kwa uso na vitisho.

Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Iran

Waziri wa Ulinzi wa Iran amebainisha kwamba, jeshi la Iran na kwa azma na utayarifu wake kamili, sambamba na kubaini vizuizi limempa adui ujumbe huu kwamba, iwapo atafanya uvamizi, basi atapata jibu kali. Brigedia Jenerali Amir Hatami ameashiria tofauti muhimu iliyopo kati ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na majeshi ya nchi nyingine na kusema, jeshi la Iran kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu ni la kuwahudumia wananchi kikamilifu na linalotokana na wananchi, lakini katika nchi nyingine jeshi si tu kuwa ni la ulinzi  moja kwa moja na lisilowahudumia raia, bali ni la kuwahudumia watawala na viongozi.

Tags