Israel inajaribu kuanzisha kituo cha kijeshi Somaliland
(last modified 2024-10-21T07:21:24+00:00 )
Oct 21, 2024 07:21 UTC
  • Israel inajaribu kuanzisha kituo cha kijeshi Somaliland

Tovuti ya habari ya Qatar, Middle East Monitor imeripoti kuwa Israel inajaribu kuanzisha kituo cha kijeshi huko Somaliland kwa lengo la kudhibiti njia ya usafiri katika Bahari Nyekundu.

Kuna uwezekano wa hilo kuthibiti kwa kutilia maanani kuwa Israeli ina mipango ya kuitambua rasmi Somaliland, kama nchi huru.

Eneo hilo liko kwenye Ghuba ya Aden na linapakana na Ethiopia, Somalia na Djibouti na linahesabiwa kuwa eneo la kimkakati kijiografia ambalo lina kilomita 740 za ukanda wa pwani kwenye Ghuba ya Aden.

Somaliland inapatikana katika Ghuba ya Aden, karibu na lango-bahari la Bab al-Mandeb. Takriban theluthi moja ya mizigo inayosafirishwa kwa njia ya bahari duniani hupitia lango hilo.