-
Meja Jenerali Safavi: Zama za kusambaratika nguvu za Marekani zimewadia
Apr 02, 2020 02:42Msaidizi na Mshauri wa ngazi za juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran amesema kuwa, zama za kusambaratika nguvu za kisiasa na kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla zimewadia.
-
Kosa dogo kabisa la maadui waovu dhidi ya Iran litakuwa mwisho wao
Apr 02, 2020 01:52Katika siku hizi viongozi wa serikali yenye kinyongo ya Marekani wameendeleza uhasama wao wa miaka 41 sasa dhidi ya taifa la Iran.
-
Rouhani: Marekani imepoteza fursa ya kihistroria ya kusahihisha makosa yake
Apr 01, 2020 21:55Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani imepoteza fursa ya kipekee na ya kihistoria ya kusahihisha makosa yake kwa kukataa kulindolea taifa hili vikwazo haramu wakati huu ambapo Iran inakabiliana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwana virusi vya corona.
-
Wagonjwa wa corona waliopata nafuu nchini Iran wapindukia 15,000
Apr 01, 2020 07:54Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa watu 15,473 wameshapata nafuu kikamilifu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kutoka hospitalini humu nchini.
-
SEPAH: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaelekea kuunda ustaarabu mpya duniani
Mar 31, 2020 21:53Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesema kuwa, baada ya kupita miaka 41 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa na licha ya kuweko njama, mashinikizo na vikwazo vya kila upande, Jamhuri ya Kiislamu inaelekea kuunda ustaarabu mpya duniani.
-
Diplomasia ya Dakta Zarif; kuweka bayana utambulisho wa kweli na mwenendo wa Marekani ulio dhidi ya ubinadamu
Mar 31, 2020 21:51Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria katika makala yenye anuani “Piganeni na virusi vya Corona, siyo na sisi” iliyochapishwa na gazeti la Kommersant la Moscow Russia juu ya mlipuko wa virusi vya Corona kote ulimwenguni na kuandika: “Zama za kukaa na kuangalia utunishaji misuli wa Marekani zimepita.”
-
Wagonjwa wa corona waliopata nafuu nchini Iran wapindukia 14,656
Mar 31, 2020 11:25Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa: Hadi leo Jumanne mchana watu 14,656 miongoni mwa walioambukizwa kirusi cha corona wamepata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitali.
-
Rezai: Hatua yoyote ya kijeshi itakayochukua Marekani Iraq ni sawa na shambulio linalofanywa na DAESH (ISIS)
Mar 31, 2020 11:23Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema, hatua yoyote ya kijeshi itakayochukua Marekani nchini Iraq itakuwa sawa na hujuma inayofanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).
-
Watoto wenye umri wa chini zaidi wapata nafuu kikamilifu baada ya kuugua corona nchini Iran
Mar 30, 2020 23:17Watoto wawili wachanga wa Kiirani wamekuwa watu wenye umri mdogo zaidi kupona corona humu nchini baada ya kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19. Tukio hilo limetokea katika mkoa wa Gilan wa kaskazini mwa Iran.
-
Kiongozi Muadhamu asisitiza umuhimu wa kufanywa uchunguzi wa afya kwa ajili ya kukabiliana na corona
Mar 30, 2020 07:32Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali khamenei Jumapili ya jana alimwandikia barua Waziri wa Afya wa Iran akipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na wafanyakazi na wadau wa masuala ya afya hapa nchini na kusema kuwa, uchunguzi wa afya unaofanyika nchini kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya corona ni kazi kubwa na adhimu.