Kosa dogo kabisa la maadui waovu dhidi ya Iran litakuwa mwisho wao
Katika siku hizi viongozi wa serikali yenye kinyongo ya Marekani wameendeleza uhasama wao wa miaka 41 sasa dhidi ya taifa la Iran.
Rais Donald Trump wa nchi hiyo ameendelea kupiga hatua katika njia isiyo sahihi na kuona ndoto za mchana kwamba, anaweza kuitia hofu na woga Iran kwa kutoa vitisho na hatimaye kuilazimisha isalimu amri.
Kutokana na hatua hiyo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) limetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya tarehe 12 Farvardin, Siku ya Jamhuri ya Kiislamu, likitilia mkazo stratijia ya kuendelea kusimama kidete, muqawama na kustawisha uwezo wa kujihami na kusema: 'Kosa dogo kabisa la maadui waovu katika nukta yoyote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu litakuwa la mwisho la maadui hao. Taarifa hiyo imesema kuwa: "Jibu madhubuti na haribifu la kambi ya Mapinduzi ya Kiislamu halitasawariki na halitawapa maadui hata fursa ya kujutia."
Uzoefu umeonyesha kuwa, uhasama wa Marekani dhidi ya Iran hauna kikomo kwa sababu ni sehemu ya utambulisho na dhati ya kibeberu ya utawala wa Marekani. Suala hili limeelezwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika minasaba tofauti na kusisitiza kuwa: Marekani daima imekuwa ikisaka fursa ya kulitwisha taifa la Iran matakwa na malengo yake.
Tunaweza kusema kuwa, mahesabu yaliyojaa makosa yamekuwa yakiifanya Marekani ichukue maamuzi yenye makosa ambayo matokeo yake yamekuwa kinyume na matarajio ya viongozi wa White House. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, maadui hao hawana uelewa sahihi kuhusiana na uwezo wa taifa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Katika mwendelezo wa mahesabu hayo alili na yenye makosa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amehalalisha vikwazo vya kidhalimu vya nchi hiyo dhidi ya Iran na kudai kuwa, 'Tehran inataka kufutiwa vikwazo na kuachiliwa fedha zake kwa kutumia kisingizio cha kukabiliana na corona'.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ha Iran, Sayyid Abbas Mousavi amejibu matamshi hayo yaliyojaa chuki ya Pompeo akisema: Serikali ya Marekani haina hadhi ya kutoa maoni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Iran kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema katika miaka ya hivi karibuni serikali ya Marekani imekiri kuwa kwa uchache imetumia dola trilioni 9 kwa ajili ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi za magharibi mwa Asia na kuvuruga utulivu wa eneo hilo na kuongeza kuwa: "Fedha hizo zote zingeweza kutumiwa kwa ajili ya raia wa Marekani ili walimwengu wasishuhudie vilio vya wauguzi wa Kimarekani wanaohuzunishwa na uhaba wa vitendea kazi vya tiba na manung'uniko ya wafanyakazi wa sekta ya afya katika nchi hiyo inayodai kuwa na hali bora na kuwa ni kinara wa haki za binadamu.”
Wakati huo huo Dr. Anthony Fauci ambaye ni Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Kuambukiza nchini Markani alisema Jumapili iliyopita katika mahojiano yake na televisheni ya CNN kwamba: Maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani yumkini yakasababisha vifo vya baina ya watu laki moja na laki mbili.
Hasira ya Marekani dhidi ya Iran ina chanzo na sababu nyingi. Marekani imekula kichapo na vipigo mara kadhaa vya Iran na hii leo inaendelea kushuhudia mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu katika nyanja mbalimbali na kusimama kidete kwa taifa la Iran licha ya vikwazo na mashaka wanayokabiliana nayo. Mafanikio kama ya kutengeneza kifaa cha Kiirani cha kupima virusi vya corona, maendeleo makubwa katika uwanja wa kutengeneza dawa za kikabiliana na virusi hivyo, utengenezaji wa chombo cha kuzalisha oksijeni na zana nyingine zinazohitajika kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya corona ni sehemu ya mafanikio ya wataalamu wa Iran kwa ajili ya kuzima na kubatilisha taathira mbaya za vikwazo haramu vya Marekani.
Ni kwa kutilia maanani hayo yote ndipo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran akasema: Asasi zote za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zikishirikiana na wananchi, zitaendeleza mapambano dhidi ya corona na kuibuka na ushindi licha ya vikwazo dhalimu, haramu na vya upande mmoja vya Marekani.