SEPAH: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaelekea kuunda ustaarabu mpya duniani
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesema kuwa, baada ya kupita miaka 41 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa na licha ya kuweko njama, mashinikizo na vikwazo vya kila upande, Jamhuri ya Kiislamu inaelekea kuunda ustaarabu mpya duniani.
Jeshi la SEPAH limetoa taarifa maalumu kwa mnasaba wa maadhimisho ya tarehe Mosi Aprili ambayo ni siku ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisita kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ni uhakika ulio hai, imara na unaotoa ilhamu kwa mataifa mengine yanayopigania ukombozi. Jamhuri ya Kiislamu imezaa fikra iliyosimama juu ya msingi wa kupigania uadilifu, haki na kupambana na ubeberu na hivi sasa fikra hiyo imepanua wigo wake katika jiografia ya ubinadamu na kuyaathiri mataifa yote huku ikilazimisha kambi ya kiistikbari hasa utawala wa kidikteta, kigaidi na Kizayuni wa Marekani kuwekwa pembeni na kuzidi kupoteza ushawishi wake katika matukio ya kiistratijia duniani.
Taarifa hiyo ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH aidha imesema, kupenya ujumbe wa kimaanawi wa Jamhuri ya Kiislamu katika nyoyo na nafsi za vijana wanaopingania ukombozi duniani ni bishara njema ya kuweko mustakbali bora na wenye matumaini ya kuweza wanadamu kukombolewa kutoka kutoka kwenye makucha ya madola ya kishetani yaliyo dhidi ya binadamu ukiwemo mfumo Marekani wa kiudanganyifu, uliojaa hila na unaochezea haki za wengine duniani.
Baada ya kupata ushindi Mapinduzi matukufu ya Kiislamu kwa uongozi wa busara na wa kishujaa wa Imam Khomeini MA mwaka 1979, muda mchache baadaye kuliitishwa kura ya moni kote nchini Iran ambapo tarehe Mosi Aptili 1979, wananchi wa Iran walipasisha kwa asilimia 98 kutawala mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu humu nchini.