Meja Jenerali Safavi: Zama za kusambaratika nguvu za Marekani zimewadia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i60115-meja_jenerali_safavi_zama_za_kusambaratika_nguvu_za_marekani_zimewadia
Msaidizi na Mshauri wa ngazi za juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran amesema kuwa, zama za kusambaratika nguvu za kisiasa na kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla zimewadia.
(last modified 2026-02-05T12:50:29+00:00 )
Apr 02, 2020 07:12 UTC
  • Meja Jenerali Safavi: Zama za kusambaratika nguvu za Marekani zimewadia

Msaidizi na Mshauri wa ngazi za juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran amesema kuwa, zama za kusambaratika nguvu za kisiasa na kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla zimewadia.

Meja Jenerali Sayyid Yahya Rahim Safavi,  amesema katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter akitoa radiamali yake juu ya uwepo usio wa kisheria wa jeshi la Marekani nchini Iraq kuwa, serikali na mamlaka ya Marekani inapaswa kuainisha taklifu yake kuhusiana na kufungamana kwake na mikataba pamoja na sheria za kimataifa.

Msaidizi na Mshauri wa ngazi za juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran ameongeza kuwa, Bunge la Iraq katika muswada wake liliopasisha mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2019 chini ya anuani ya 'kufukuzwa majeshi ya kigeni Iraq' lilitaka kuondoka nchini humo majeshi ya kigaidi ya Marekani katika ardhi ya nchi hiyo ambapo kuendelea kuweko majeshi hayo baada ya muswada huo ni nembo ya wazi kabisa ya kukiuka mamlaka ya kujitawala taifa la Iraq.

Wanajeshi wa Marekani wakiwa nchini Iraq

Aidha Meja Jenerali Sayyid Yahya Rahim Safavi amebainisha kwamba, kama serikali na mamlaka ya Marekani haifungamani na sheria pamoja na mikataba ya kimataifa inapaswa kubeba dhima ya matokeo mabaya ya uwepo wake haramu na usio wa kisheria na ukaliaji wake mabavu wa ardhi ya nchi hiyo.

Itakumbukwa kuwa, katika miezi ya hivi karibuni upinzani dhidi ya uwepo wa majeshi ya Marekani katika ardhi ya Iraq umeongezeka mno ambapo serikali ya Rais Donald Trump iko chini ya mashinikizo makubwa.