-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu udharura wa kuwa macho mbele ya njama za maadui na kuwa tayari kutoa jibu na pigo mkabala
Feb 24, 2020 03:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru wananchi kwa kuufuzu kwa kiwango cha kuridhisha mtihani mkubwa wa uchaguzi na kuweza kuzima propaganda za kila upande za maadui na kutumia kwao vibaya suala hilo na akasisitiza kwamba: Taifa zima linapaswa kuwa macho na kujiweka tayari kukabiliana na njama za adui zinazolenga kutoa pigo kwa mihimili tofauti ya nchi.
-
Iran yatengeneza kifaa cha kupima kirusi cha Corona
Feb 24, 2020 01:13Wataalamu Wairani wamefanikiwa kutengeneza kifaa maalumu cha kupima kirusi cha Corona. Kifaa hicho ni cha kwanza cha aina hiyo kuundwa nchini Iran.
-
Rais Rouhani: Vikwazo vya Marekani vinashabihiana na virusi vya corona
Feb 24, 2020 01:11Rais Hassan Rouhani amesema vikwazo vya Marekani vinafanana na virusi vya corona, ambapo wasi wasi unaozushwa navyo ni mkubwa kuliko ukweli wa mambo.
-
Wizara ya Afya: Watu 8 wameaga dunia kwa ugonjwa wa Corona nchini Iran
Feb 24, 2020 01:05Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Upashaji Habari katika Wizara ya Afya na Tiba ya Iran amesema kuwa watu wanane wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona na wengine 43 wameambukizwa maradhi hayo hapa nchini.
-
Rahmani Fadhli: Asilimia 42.57 ya wananchi wa Iran wameshiriki uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu
Feb 23, 2020 10:50Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa duru ya 11 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge ulikuwa wa asilimia 42.57.
-
Rouhani: Iran haijafunga mlango wa mazungumzo ya kuinusuru JCPOA
Feb 23, 2020 10:02Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijafunga mlango wa kufanya mazungumzo na nchi za Ulaya kwa shabaha ya kuyanusuru makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Kiongozi Muadhamu awashukuru wananchi na kusisitizia udharura wa kukabiliana na njama za maadui
Feb 23, 2020 03:45Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru wananchi kwa kuufuzu kwa kiwango cha kuridhisha mtihani mkubwa wa uchaguzi na kuweza kuzima propaganda za kila upande za maadui na kutumia kwao vibaya suala hilo na akasisitiza kwamba: Taifa zima linapaswa kuwa macho na kujiweka tayari kukabiliana na njama za adui zinazolenga kutoa pigo kwa mihimili tofauti ya nchi.
-
Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Uholanzi wakutana Tehran
Feb 22, 2020 10:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran wamekutana na kufanya mazungumzo mjini Tehran leo Jumamosi.
-
Hatua ya kisiasa ya FATF ya kuiweka Iran katika orodha nyeusi
Feb 22, 2020 08:01Nchi za Magharibi huku zikiongozwa na Marekani kwa muda sasa zimekuwa zikizingatia na kutilia maanani utekelezaji wa siasa za mashinikizo ya pande zote kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lengo likiwa ni kujaribu kubadilisha misingi na siasa za nchi hii.
-
Zoezi la kuhesabu kura za Bunge la Iran linaendelea, matokeo rasmi ya baadhi ya maeneo yameshatangazwa
Feb 22, 2020 04:02Msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran amesema kuwa zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa jana Ijumaa wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na uchaguzi mdogo wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu linaendelea na matokeo rasmi ya baadhi ya maeneo yameshatolewa.