Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Uholanzi wakutana Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59321-mawaziri_wa_mambo_ya_nje_wa_iran_na_uholanzi_wakutana_tehran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran wamekutana na kufanya mazungumzo mjini Tehran leo Jumamosi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 22, 2020 10:18 UTC
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Uholanzi wakutana Tehran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran wamekutana na kufanya mazungumzo mjini Tehran leo Jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amekutana na Stef Blok Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholani na kujadili kuhusiana na masuala ya uhusiano wa pande mbili na pia maudhui zingine.

Mkutano huo ulikuwa ni duru ya kwanza ya mazungumzo baina ya mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Uholanzi.

Inatazamiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi pia atakutana na kufanya mazungumzo na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Stef Blok Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi (kushoto)  na Abbas Rezai, Mkuu wa Mkoa wa Isfahan, kati mwa Iran

Stef Blok jana Ijumaa pia alitembelea mji wa Isfahan kati mwa Iran na kukutana na Abbas Rezai, Mkuu wa Mkoa wa Isfahan ambapo walijadiliana kuhusua masuala ya uchumi, uzalishaji wa kiviwanda na utalii.