-
Mazoezi ya kijeshi ya Iran, Russia na China yanaendelea kama ilivyopangwa
Dec 28, 2019 09:59Mazoezi makubwa ya majeshi ya pamoja ya majeshi ya majini ya Iran, Russia na China leo yameingia siku ya pili na yanaendelea kama ilivyopangwa.
-
Ali Akbar Velayati: Iran itasimama imara kukabiliana na njama chafu za maadui za kuzigawa nchi za Asia Magharibi
Dec 28, 2019 08:43Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa Iran inapinga aina yoyote ya uingiliaji wa kigeni katika masuala ya nchi za eneo la Asia Magharibi, kama ambavyo itasimama imara kukabiliana na dhulma, njama, uvamizi na ajenda chafu za maadui kwa ajili ya kuzidhoofisha na kuzigawa nchi za eneo.
-
Mousavi: Wadau wote duniani wana mchango katika zama za baada ya Magharibi
Dec 28, 2019 00:36Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "Hivi sasa, sisi tunaishi katika dunia ya baada ya enzi za Magharibi, ambapo wadau wote duniani wana mchango katika mahusiano ya zama hizo."
-
Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya Iran, China, Russia; kigezo chenye ufanisi cha kieneo kuhusu usalama
Dec 27, 2019 20:55Kufanyika mazoezi ya pamoja ya majeshi ya majini ya Iran, Russia na China katika eneo lenye umuhimu wa kistratijia la kaskazini mwa Bahari ya Hindi na Bahari ya Oman ni ushirikiano wa kieneo usiohusisha madola ajinabi.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: 9 Dei ni siku muhimu katika historia
Dec 27, 2019 08:26Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, tarehe 9 Dei mwaka 1388 Hijria Shamsia (30 Disemba 2009) ni siku muhimu sana katika historia ya binadamu.
-
Iran, Russia na China zaanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kaskazini mwa Bahari ya Hindi
Dec 27, 2019 06:21Mazoezi ya kijeshi ya baharini yanayoshirikisha majeshi ya majini ya nchi tatu za Iran, Russia na China yameanza leo Ijumaa kaskazini mwa Bahari ya Hindi kwa kaulimbiu ya "Amani, Urafiki na Usalama Endelevu Chini ya Kivuli cha Ushirikiano na Umoja".
-
Kamanda wa jeshi la Majini Iran: Marekani haina uthubutu wa kuivamia kijeshi Iran
Dec 26, 2019 22:52Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran amesema kuwa Wamarakeni wana umaarufu wa kufanya uvamizi dhidi ya nchi mbalimbali lakini kutokana na uwezo na utayarifu wa jeshi la nchi hii, hawana uthubutu wa kuivamia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kiongozi Muadhamu: Kuna njama maalumu za kusahaulisha utamaduni wa jihadi na kufa shahidi
Dec 26, 2019 08:33Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, suala la kuwaenzi mashahidi ni jambo la lazima na ni jukumu la kila mtu kwani hivi sasa kuna siasa na harakati za kikhabithi zinazolenga kusahaulisha nembo za Mapinduzi ya Kiislamu hususan utamaduni wa jihadi na kuwa tayari kujitolea kufa shahidi katika njia ya Allah.
-
Rouhani: Tumepata njia mpya za kufanya biashara na nchi mbalimbali
Dec 25, 2019 21:42Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa leo hii Iran imepata njia mpya za kufanya biashara na nchi mbalimbali za dunia na kwamba imepiga hatua mpya katika uwanja huo na nchi kama India, Malaysia, Uturuki, China na Russia.
-
Rais Rouhani: Mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani hayalilengi taifa la Iran pekee
Dec 25, 2019 09:12Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani hayalilengi taifa la Iran pekee, bali kuna mataifa mengine ya dunia ambayo nayo yanaandamwa na siasa hizi za Washington za kuzishinikiza kiuchumi nchi nyingine.