-
Zarif: Wairani hawatasalimu amri mbele dhulma za Marekani
Nov 02, 2019 03:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezungumzia vikwazo vipya vya Marekkani dhidi ya Iran na kusema kuwa, hata kama Marekani itawawekea vikwazo wanaume, wanawake na watoto wote wa Iran kamwe Wairani hawatasalimu amri na kupiga magoti mbele ya serikali ya Washington.
-
Ayatullah Movahedi-Kermani: Marekani ndiye muhusika mkuu wa matatizo ya Iraq
Nov 01, 2019 10:28Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria matukio yanayoendelea hivi sasa nchini Iraq na kusisitiza kwamba tangu miaka 16 iliyopita, serikali ya Marekani ilikuwa ikiiba zaidi ya mapipa milioni moja ya mafuta ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa kisingizio cha kufidia gharama za vita.
-
IRGC: Uvamizi wowote dhidi ya Iran utakabiliwa na jibu kali
Oct 31, 2019 10:38Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema jaribio lolote la maadui la kujaribu kuvamia ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litapokea jibu kali.
-
Usalama na udharura wa kuulinda, kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Oct 31, 2019 04:11Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran alisema jana katika hotuba yake katika Hafla ya 17 ya Pamoja ya Kuhitimu Maafisa wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Anga kwamba, kulinda usalama ni jukumu tukufu na nyeti la vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza udharura wa kuwa tayari zaidi kiulinzi katika kukabiliana na maadui.
-
Dakta Zarif: Kumeanza harakati ya kuelekea katika utawala wa kisheria Syria
Oct 31, 2019 04:11Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, baada ya miaka kadhaa ya vita haribifu, hatimaye kwa juhudi za mchakato wa mazungumzo ya Astana kumeanza harakati ya kuelekea katika utawala wa kisheria nchini Syria.
-
Vaezi: Lengo la Marekani, Saudia na utawala wa Kizayuni ni kudhoofisha serikali za Iraq na Lebanon
Oct 30, 2019 08:44Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matukio ya sasa katika nchi za Iraq na Lebanon na kusema kuzidhoofisha serikali huru ni kati ya malengo ya Marekani, Saudia na Utawala wa Kizayuni.
-
Kiongozi Muadhamu: Watu wa Iraq, Lebanon wafuatilie matakwa yao ya haki kwa njia za kisheria
Oct 30, 2019 08:32Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria njama za maadui za kuvuruga usalama katika baadhi ya nchi za eneo na kusema: "Wanaojali Iraq na Lebanon wafahamu kuwa, kipaumbele chao kinapaswa kuwa kuondoa hali ya ukosefu wa usalama na wananchi wa nchi hizo nao wafahamu kuwa, matakwa yao ya haki yanaweza tu kukidhiwa katika fremu ya mfumo wa kisheria."
-
Zarif: Trump hawezi kuilazimisha Iran iafiki mpatano ya upande mmoja
Oct 30, 2019 00:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: "Serikali ya Marekani haiwezi kuilazimisha Iran iafiki mapatano ya upande mmoja."
-
Iran yalikosoa Baraza la Usalama la UN kwa kuzembea mbele ya jinai za Israel
Oct 29, 2019 08:22Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameituhumu jamii ya kimataifa kwamba imefeli mbele ya sera za kujipanua za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Palestina.
-
Mhimili wa Muqawama; ushindi katika medani ya vita dhidi ya maadui Asia Magharibi
Oct 29, 2019 08:14Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mhimili wa muqawama katika eneo la Asia Magharibi ndiyo sababu ya kushindwa maadui na hivyo kuwafanya waanze kufanya njama dhidi ya harakati ya muqawama na eneo hili la Asia Magharibi.