Zarif: Trump hawezi kuilazimisha Iran iafiki mpatano ya upande mmoja
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56936-zarif_trump_hawezi_kuilazimisha_iran_iafiki_mpatano_ya_upande_mmoja
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: "Serikali ya Marekani haiwezi kuilazimisha Iran iafiki mapatano ya upande mmoja."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 30, 2019 00:49 UTC
  • Zarif: Trump hawezi kuilazimisha Iran iafiki mpatano ya upande mmoja

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: "Serikali ya Marekani haiwezi kuilazimisha Iran iafiki mapatano ya upande mmoja."

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliyasema hayo Jumanne katika mahojiano na Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar na kwa mara nyingine kutoa wito kwa nchi za eneo kujenga hali ya kuaminiana baina yao. Zarif ameongeza kuwa: "Vita havitakuwa kwa manufaa ya yeyote".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Iran imeziomba nchi za eneo kujenga hali ya kuaminiana chini ya mwavuli wa 'Ubinifu wa Hormoz". 

Rais Hassan Rouani wa Iran akihutubu katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Mnamo Septemba 25, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasilisha mpango mpya wa amani katika eneo la Ghuba ya Uajemi ambao unajulikana kama 'Ubunifu wa Amani wa Hormuz' kwa kifupi HOPE katika hotuba yake kwenye mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York.

Nchi kadhaa tayari zimetangaza kuunga mkono mpango huo wa amani wenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kieneo kwa ajili ya kulinda amani na uthabiti katika Ghuba ya Uajemi.