-
Iran yakosoa ukatili wa Marekani wa kumzuia Zarif kumtembelea balozi hospitalini
Sep 28, 2019 07:41Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amekosoa vikali kitendo cha kikatili cha Marekani cha kumzuia Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kumtembelea Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ambaye amelazwa hospitalini mjini New York.
-
Rouhani: Nchi za Ulaya zimekiri hazijui aliyeshambulia Aramco
Sep 27, 2019 23:10Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema licha ya nchi za Ulaya kuituhumu Tehran kuwa imehusika katika mashambulizi yaliyolenga kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia, lakini viongozi wa nchi hizo wamekiri wazi kuwa hawajui ni nani aliyetekeleza hujuma hizo.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Hatuna matumaini wala imani na nchi za Ulaya
Sep 27, 2019 09:10Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa utendaji wa nchi za Ulaya baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema si tatizo kukutana na kufunga mikataba na nchi hizo lakini hatupaswi kuwa na matumaini wala kuziamini nchi hizo.
-
Sheikh Siddiqi: Kujihami kutakatifu taifa la Iran kumeacha athari katika historia ya leo
Sep 27, 2019 09:07Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, miaka minane ya kujihami kutakatifu taifa la Iran mbele ya uchokozi wa utawala wa dikteta Saddam wa Iraq kumeacha athari katika historia ya leo.
-
Meli ya Uingereza iliyokuwa inashikiliwa na Iran, yaruhusiwa kuondoka Bandar Abbas
Sep 27, 2019 03:27Meli ya mafuta ya Uingereza ya Stena Impero imeruhusiwa kuondoka bandarini huko Bandar Abbas, kusini mwa Iran na kuelekea kwenye maji ya kimataifa.
-
Iran yaitaka Uingereza iache ukhabithi na ushetani wake wa kuingilia mambo ya wengine
Sep 26, 2019 23:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Uingereza inapaswa kuacha ukhabidhi na ushetani wake wa kuingilia masuala ya eneo la Mashariki ya Kati na kuwauzia silaha wavamizi wa Yemen pamoja na kushiriki katika jinai dhidi ya binadamu ambazo zimethibitishwa pia na Umoja Mataifa.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Ahadi za nchi za Ulaya ni tupu
Sep 26, 2019 10:57Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza namna malengo ya uadui wa nchi za Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kimsingi yasivyo na tofauti na ya adui Marekani na kueleza kuwa: Nchi za Ulaya kidhahiri zinajidhihirisha kuwa patanishi na kusema maneno mengi lakini yote hayo ni maneno matupu.
-
Zarif: Iran iko tayari kufikia maelewano na nchi za eneo kuhusu "Ubunifu wa Amani ya Hormuz"
Sep 26, 2019 04:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kikamilifu kufanya mazungumzo na kufikia maelewano na nchi za eneo na Umoja wa Mataifa kuhusu mpango iliopendekeza wa kudhamini amani ya Ghuba ya Uajemi.
-
Rais Rouhani: Katu hatutofanya mazungumzo na adui chini ya vikwazo
Sep 25, 2019 12:52Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ni jambo lisiloyumkinika kwa taifa hili kufanya mazungumzo na adui likiwa chini ya mashinikizo na vikwazo vya kidhalimu na vilivyo kinyume cha sheria.
-
Rais Rouhani: Kama Trump anataka mazungumzo na Iran arekebishe kwanza yote aliyoyaharibu
Sep 25, 2019 04:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kama kweli rais wa Marekani, Donald Trump anataka mazungumzo na Iran, anapaswa kabla ya jambo lolote arejeshe kwanza imani ya taifa hili aliyoipoteza.