Meli ya Uingereza iliyokuwa inashikiliwa na Iran, yaruhusiwa kuondoka Bandar Abbas
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56269-meli_ya_uingereza_iliyokuwa_inashikiliwa_na_iran_yaruhusiwa_kuondoka_bandar_abbas
Meli ya mafuta ya Uingereza ya Stena Impero imeruhusiwa kuondoka bandarini huko Bandar Abbas, kusini mwa Iran na kuelekea kwenye maji ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 27, 2019 03:27 UTC
  • Meli ya Uingereza iliyokuwa inashikiliwa na Iran, yaruhusiwa kuondoka Bandar Abbas

Meli ya mafuta ya Uingereza ya Stena Impero imeruhusiwa kuondoka bandarini huko Bandar Abbas, kusini mwa Iran na kuelekea kwenye maji ya kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, mapema leo asubuhi, meli hiyo imeondoka Bandar Abbas na kuelekea kwenye maji ya kimataifa.

Kabla ya hapo, Hamid Baeidinejad, Balozi wa Iran mjini London alisema siku ya Jumatatu kuwa meli ya Stena Impero ya Uingereza imesharuhusiwa kuondoka nchini Iran.

Wafanyakazi wa meli ya mafuta ya Uingereza ya Stena Impero walioachiliwa huru tarehe 4 Septemba mwaka huu kama njia ya kuonesha huruma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

Tarehe 19 Julai mwaka huu, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH liliizuia meli ya mafuta ya Uingereza katika mkoa wa Hormozgan baada ya Taasisi ya Bandari na Safar za Majini ya mkoa huo kuliomba jeshi hilo kufanya hivyo. Moja ya makosa yaliyofanywa na meli hiyo ya mafuta ya Uingereza lilikuwa ni kuzima kifaa cha kuonesha ilipo, suala ambalo lilihatarisha mno usalama wa vyombo vingine.

Mabaharia wa meli hiyo waliachiliwa huru tarehe 4 Septemba mwaka huu kama njia ya kuonesha huruma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za usafiri wa baharini na makubaliano ya haki za baharini ya mwaka 1982, meli moja ya kijeshi inaweza kuizuia meli isiyo ya kijeshi katika maji huru iwapo maeli hiyo itakataa kuchunga na kuheshimu sheria za kimataifa.