-
Rouhani: Ni lazima Marekani iachane na sera zake za vita na mashinikizo
Sep 11, 2019 23:37Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, stratijia ya taifa la Iran katika kukabiliana na mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi ni kusimama kidete. Ameongeza kuwa: "Ni lazima Marekani iweke kando sera zake za kupenda vita na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa."
-
Zarif akosoa tangazo la kushadidishwa ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya Iran
Sep 11, 2019 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa tangazo la kushadidishwa ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya Iran na kusema: "Kiu cha vita kinapaswa kuondoka pamoja na mpenda vita mkuu ."
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa familia za Mashahidi wa Karbala
Sep 11, 2019 03:05Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Iraq na familia za Mashahidi kufuatia tukio la kufa shahidi makumi ya watu katika mji mtakatifu wa Karbala.
-
Iran: Hatufanyi mazungumzo na Marekani iwapo wanaendeleza ugaidi wa kiuchumi
Sep 11, 2019 02:59Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema ni jambo lisilowezekana kwa Jamhuri ya Kiislamu kufanya mazungumzo na Marekani madhali serikali ya Washington inaendeleza ugaidi wa kiuchumi na kuliwekea vikwazo taifa hili.
-
Zarif amwambia Trump, kaulimbiu ya Netanyahu ni: Tutapigana vita hadi askari wa mwisho wa Marekani
Sep 10, 2019 22:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemtumia ujumbe wa Twitter Rais Donald Trump wa Marekani akisema: Kaulimbiu ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ni: Tutapigana vita hadi atakapobakia askari wa mwisho kabisa wa Marekani.
-
Iran ya Kiislamu yaghariki katika maombolezo ya Siku ya Ashura
Sep 10, 2019 08:21Mamilioni ya wananchi wa Iran, leo Jumanne wameadhimisha kwa shauku na hamasa kubwa siku ya maombolezo makubwa ya Ashura, kukumbuka siku aliyouawa shahidi kidhulma Bwana wa Mashahidi, mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW, Imam Husain AS katika jangwa la Karbla (la Iraq ya leo).
-
Muhuri wa IAEA wa kuunga mkono makubaliano ya JCPOA na mchezo mpya wa maigizo wa Netanyahu
Sep 10, 2019 06:09Baada ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomikia (IAEA) kutoa ripoti yake mpya inayotathmini hatua za Iran katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ameibuka tena na kudai kuwa, miradi ya nyuklia ya Iran ni ya kijeshi na kwamba, eti taifa hili linataka kutengeza bomu la atomiki.
-
Zarif: Israel, mwana kilizi, ndiye mmiliki halisi wa silaha za nyuklia
Sep 10, 2019 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu matamshi ya kijuba ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, aliyedai kuwa ana ushahidi mpya unaoonesha kuwa Tehran inaunda kwa siri silaha za nyuklia; ambapo amesema kauli hiyo ya kichochezi ya Benjamin Netanyahu inalenga kufanikisha ajenda ya vita ya utawala huo haramu.
-
Mwakilishi wa Iran UN: Marekani imekiuka mkataba wa NPT
Sep 09, 2019 22:08Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ametilia mkazo jukumu la pamoja la kupiga marufuku aina yoyote ya majaribio ya uripuaji silaha za nyuklia na kueleza kwamba Marekani imekiuka mkataba wa kuzuia uundaji na uenezaji silaha za nyuklia (NPT) kwa kujitoa kwenye makubaliano yanayohusiana na mkataba huo na kwa kuanzisha mashindano ya kuzifanya silaha hizo za nyuklia kuwa za kisasa zaidi.
-
Iran ya Kiislamu yaghariki kwenye maombolezo ya Tasua ya Imam Hussein (as)
Sep 09, 2019 12:14Katika Siku ya Tasua, Iran ya Kiislamu leo ilighariki kwenye dimbwi la huzuni na majonzi ya maombolezo ya Imam Hussein (as), Imam wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia pamoja na masahaba zake waaminifu.