-
JCPOA katika barabara ya upande mmoja ya Iran kupunguza uwajibikaji wake
Sep 09, 2019 05:27Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran amesema: "Mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) si barabara ya upande mmoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua maamuzi yanayofaa wakati utakapowadia."
-
Zarif awataka wavamizii 'walioshindwa' nchini Afghanistan waondoke
Sep 09, 2019 02:47Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuhusiana madola ya kigeni kuitumia vibaya hali ya sasa nchini Afghanistan na kuvitaka vikosi vya kigeni ambavyo vimeshindwa kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Zarif: Wakala wa IAEA ufanye kazi kitaalamu bila ya upendeleo
Sep 08, 2019 20:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unapaswa kutekeleza majukumu yake kitaalamu, kwa usiri na bila ya kupendelea upande wowote.
-
Mamilioni washiriki kumbukumbu ya Tasua Iran na maeneo mengine ya dunia
Sep 08, 2019 23:20Mamilioni ya Waislamu wa Iran na maeneo mengine ya dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 9 Mfunguo Nne Muharram wameshiriki katika vikao, majlisi na shughuli za maombolezo na kukumbuka misiba na masaibu yaliyomkuta mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw), Imam Hussein bin Ali (as), ndugu na mswahaba zake waaminifu huko Karbala nchini Iraq mwaka 61 Hijria.
-
Ayatullah Hamedani awataka Waislamu wa Kashmir waendeleze muqawama
Sep 08, 2019 07:48Mwanachuoni mashuhuri hapa nchini Iran sambamba na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuwaunga mkono Waislamu wanaodhulumiwa wa eneo la Kashmir, amewataka Wakashmir waendelee kusimama kidete na kudumisha moyo wa muqawama.
-
Hatua ya tatu ya Iran ya kupunguza uwajibikaji wake ndani ya JCPOA; kuingia katika marhala ya mwisho ya kutekeleza majukumu yake ya kiufundi
Sep 08, 2019 03:14Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tarehe saba Julai mwaka huu ilianza mchakato wa kuvuka kiwango cha urutubishaji urani cha asilimia 3.67 baada ya kumalizika muhula wake wa siku 60 iliokuwa imeutoa kwa nchi za Ulaya kutekeleza ahadi zao kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Kaimu wa wakala wa Umoja wa Mataifa wa Nishati ya Atomiki safarini Tehran
Sep 08, 2019 02:55Cornel Feruta Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA yuko safarini Tehran kwa lengo la kukutana na wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kamalvandi: Mashinepewa (centrifuges) za kisasa za nyuklia za Iran zaanza kufanya kazi + Video
Sep 07, 2019 08:28Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, awamu ya tatu ya kupunguza Iran kutekeleza ahadi zake ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA ilianza jana Ijumaa kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran yatuma salamu za rambirambi Zimbabwe kufuatia kifo cha Robert Mugabe
Sep 07, 2019 03:39Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa familia, taifa, serikali na wananchi wa Zimbabwe kufuatia kifo cha baba wa taifa hilo Robert Mugabe aliyefariki dunia hapo jana.
-
Dakta Zarif: Iran na Indonesia zina mtazamo mmoja kuhusu kadhia ya Palestina
Sep 06, 2019 22:08Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran na Indonesia zina mtazamo mmoja kuhusiana na kadhia ya Palestina na kubainisha kwamba, Baytul-Muqaddas ni kibla cha kwanza cha Waislamu.